[Latest Updates]: Utoroshaji wa Madini Wadhibitiwa Mkoani Katavi

Tarehe : April 10, 2023, 9:48 a.m.
left

Na Mwanahamisi Msangi, Katavi

 Aprili 10, 2023

TUME ya Madini Mkoa wa Katavi imeweka mikakati ya kudhibiti mianya ya utoroshaji madini  kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi hivyo, kuongeza kiwango cha makusanyo ya Serikali.

Mikakati hiyo imebainishwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Andrew Mwalugaja wakati wa mahojiano maalumu yaliyofanyika mkoani Katavi kwa lengo la kuandaa kipindi maalum na makala ya  kuelimisha umma kuhusu Sekta ya Madini.

Mhandisi Mwalugaja ametaja mikakati hiyo kuwa  ni pamoja na kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi maeneo ya migodi ili kudhibiti utoroshaji  wa madini, hivyo Serikali kupata mapato yake stahiki hivyo Sekta ya Madini kuendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Mjiolojia wa Mgodi wa Katavi, Abrahman Said akielezea namna mgodi unavyotekeleza kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini amesema  kuwa  mgodi umeajiri watanzania kwa asilimia 95 wakiwemo wanawake na wanaume  pamoja na ushiriki wa uboreshaji wa huduma za  jamii kwa kuchangia shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa darasa katika shule ya msingi Magula.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals