[Latest Updates]: Tanzania Kujengwa Mtambo Mkubwa wa Uchenjuaji Madini ya Kinywe Utakaozalisha Tani 500 hadi 600 kwa Siku

Tarehe : Feb. 6, 2024, 7:55 a.m.
left

 

●Mtambo wa Uchenjuaji ulianza kujengwa 2022

●Utazalisha Madini kinywe yenye ubora wa asilimia 97.

●Majaribio ya uzalishaji yataanza rasmi mwezi machi 2024.

Na.Samwel Mtuwa - MoM

Tanzania imebarikiwa kuwa na madini ya Kinywe (Graphite) katika mikoa  mbalimbali ukiwemo mkoa wa Tanga ,Lindi na Morogoro.

Uwekezaji katika sekta ya madini nchini  unaendelea kukua kwa kasi ambapo kwasasa Tanzania inatarajia kuwa na mtambo mkubwa wa uzalishaji madini kinywe unaojengwa na Kampuni ya GodMwanga Gems Limited mkoani Tanga.

Akielezea maendeleo ya ufungaji wa mtambo meneja uzalishaji katika Mgodi huo Henry Mbando alimwelezea Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa juu ya  ubora wa mtambo wa kuchenjua madini hayo,  kuwa  mtambo huo utachenjua madini  kutoka katika  miamba na utazalisha kiasi cha tani 500 - 600 kwa siku.

Mbando alifafanua kuwa mtambo unaofungwa una uwezo wa kusaga tani 6000 za mwamba wa madini ya  kinywe na utachenjua ili kupata ubora wenye asilimia 97 ya madini ya kinywe.

Akielezea juu ya mpango wa ulipaji kodi kupitia uzalishaji huo Mbando  alifafanua kuwa ulipaji wa kodi kwa mwezi utafanyika kulingana  uzalishaji ambapo  asilimia tatu ya kodi ya mrabaha itakuwa kiasi cha Tshs.546,000,000, asilimia moja ya kodi ya ukaguzi   itakuwa Tshs.182,000,000 na kodi ya service levy  yenye asilimia sifuri nukta tatu itakuwa Tshs 54,600,000.

Kuhusu mchango wa kampuni kwa jamii (CSR)  Mbando alisema mpaka sasa  tayari ujenzi wa zahanati na nyumba ya mganga wenye thamani ya Tshs.200,000,000 umefanyika.

Changamoto kubwa ya mradi huo  iliyotolewa na uongozi wa mgodi ni kukosekana kwa nishati ya umeme ya uhakika na ubovu wa miundombinu ya barabara ambapo uongozi  umeiomba serikali kuwasaidia.

#MadiniNiMaishaNaUtajiri
# InvestTzMiningSector
#MadiniYetuYatatutoa

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals