[Latest Updates]: Mavunde apongeza Uwekezaji Maabara ya MSA Geita

Tarehe : Sept. 27, 2023, 8:14 a.m.
left

• Inapima Sampuli za Madini kwa Mionzi (PhotoAssay)

• Inatoa majibu ndani ya masaa mawili

• Asilimia 99.8 ya Wafanyakazi ni Watanzania

Zaidi ya Shilingi  Bilioni 5 zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS inayomiliki Maabara ya  upimaji wa sampuli za Madini kwa kiwango cha kimataifa mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa  Septemba 27 , 2023 na Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya MSALABS Mugisha Lwekoramu  wakati wa ufunguzi wa Maabara hiyo.

Akizungumzia kuhusu teknolojia inayotumika katika Maabara hiyo Lweramu amesema Maabara   inatumia teknolojia ya kisasa ya upimaji wa sampuli kwa njia ya mionzi yaani (PhotoAssay) ambayo ni rafiki kwa utunzaji mazingira kwasababu haitumii kemikali au moto katika upimaji sampuli.

Akielezea kuhusu ufanisi wa teknolojia hiyo , Lwekoramu amesema ni sehemu ya mapinduzi ya teknolojia kwasababu  inamwezesha mdau kupata majibu ya sampuli ndani ya masaa mawili ni tofauti  ukilinganisha na teknolojia ya zamani ya kutumia moto na kemikali.

Kwa upande , wake Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Maabara hiyo kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini , akiwataka kuendelea kufungua matawi mengine nchini.

Aidha , amewapongeza pia kwa kuweza kuajiri watanzania kwa asilimia 99.8 akiamini kuwa wafanyakazi hao wataendelea kujifunza utumiaji wa teknolojia hiyo na kutoa ujuzi huo kwa watanzania wengine.

Mhe .Mavunde, ameahidi kuwa Serikali awamu ya sita itaendelea kuwatengenezea mazigira rafiki ya uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa jinsi itakavyohitajika katika mnyororo mzima wa sekta 

Awali , Mhe .Mavunde alitembelea kampuni ya Blue Coast inayotoa huduma   migodini kama vile Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa lengo la kuangalia maendeleo ya uwekezaji.

Katika shughuli hizo , Mhe.Waziri aliambatana na  Katibu Mkuu Wizara ya Madini,Mkuu wa Mkoa Geita , Mkuu wa Wilaya ya Chunya , Mtendaji Mkuu wa GST na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals