[Latest Updates]: Wadau Sekta ya Madini Waendelea Kutoa Maoni Marekebisho ya Sheria

Tarehe : Aug. 2, 2023, 2:30 p.m.
left

DC Simanjiro aongoza Kikao Kazi kupokea Maoni ya Wadau Sekta ya Madini

Wizara ya Madini imeendelea kupokea Maoni ya Wadau wa sekta hiyo kuhusu mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria na baadhi ya Kanuni zitakazosimamia shughuli za Sekta ya Madini.

Akiongoza Kikao Kazi kinachoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dkt. Suleiman Serera amewataka wadau wa Sekta ya Madini kuchangia mawazo yao kwa uhuru ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika shughuli za sekta hiyo.

Aidha, Dkt. Serera ameyataja maeneo yatakayopokelewa mapendekezo yake na kujadiliwa leo ni pamoja na Kanuni ya Madini Ushiriki wa Serikali za Mwaka 2022, Kanuni ya Eneo Tengefu la Mirerani za Mwaka 2022, Kanuni ya Haki Madini za Mwaka 2018, Kanuni ya Masoko ya Madini za Mwaka 2019 pamoja na Kanuni za Uongezaji Thamani Madini za Mwaka 2020.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi upande wa Mazingira, Mhandisi Ally Samaje amezitolea  ufafanuzi Kanuni mbalimbali zinazopendekezwa ambapo amesema kuna baadhi ya Kanuni zina changamoto katika utekelezaji wake ambapo suluhisho lake ni kuzifanyia Marekebisho.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals