[Latest Updates]: Lindi imefunguka Mradi wa Uchimbaji Madini ya Kinywe mbioni kuanza

Tarehe : June 23, 2023, 10:14 a.m.
left

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Kijiji cha Namangale katika Halmashauri ya Mji wa Mtama Mkoani Lindi kutoa ushirikiano kwa mwekezaji wa Madini ya Kinywe Volt Resources Limited ili aweze kulipa fidia kwenye maeneo yatakayo jengwa mgodi.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Juni 18, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Namangale Mkoani Lindi ambapo amesema mgodi huo utasaidia kuongeza ajira na kuchochea maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho kupitia shughuli za uchimbaji madini.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Biteko amesema Kampuni ya Volt Resources Limited kutoka nchini Australia itakayochimba madini hayo inatarajiwa kuwekeza zaidi ya Dola za Marekani milioni 40 katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa mgodi huo ambapo inakadiriwa kuwa na hifadhi ya zaidi ya tani milioni 461 za madini ya Kinywe katika kijiji cha Namangale Mkoani Lindi.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameiomba Wizara ya Madini kuisimamia kwa karibu Kampuni ya Volt Resources Limited ili kuhakikisha mradi wa uchimbaji wa madini ya Kinywe katika kijiji cha Namangale unaharakishwa ili wananchi wa Mkoa wa Lindi wapate ajira. 

Pamoja na mambo mengine, Nauye amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameufungua mkoa wa Lindi ambapo kwa sasa Taifa linashuhudia miradi mingi ya maendeleo ikifanyika mkoani humo ukiwemo mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe unaotarajiwa kujengwa katika kijiji cha Namangale.

Katika ziara hiyo Dkt. Biteko ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unaanza kulipa fidia wananchi ili uanze uzalishaji kwa wakati.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals