[Latest Updates]: Lindi Jumbo Kuzalisha Tani 40000 za Madini Kinywe kwa Mwaka

Tarehe : June 13, 2025, 5:35 p.m.
left

LINDI JUMBO KUZALISHA TANI 40,000 ZA MADINI KINYWE KWA MWAKA

Utafiti umebaini uwepo wa tani milioni 5.5 za madini kinywe.

Uzalishaji utadumu kwa miaka 24.

Zaidi ya Wafanyakazi 290 wameajiriwa.

Ruangwa, Lindi

Imeelezwa kwamba kampuni ya  Lindi Jumbo inayojishughulisha na uchimbaji wa madini kinywe mkoani Lindi imetabanaisha kuwa ina uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani 40,000 za madini hayo kwa mwaka ikiwa pamoja na uchakataji.

Hayo yamesemwa leo Juni 13, 2025 na Paul Shauri ambaye ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Lindi Jumbo inayoshiriki katika maonesho ya madini na fursa za uwekezaji yanayoendelea  wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Shauri amesema kuwa, mgodi wa Lindi Jumbo unazalisha aina mbalimbali  za madini kinywe ikiwemo Super Jumbo, Jumbo large na Jumbo fine ambazo zinapangiliwa  kulingana na ukubwa wa punji za madini yanayozalishwa.

Akielezea kuhusu muda utakaodumu katika uzalishaji wa madini hayo , Shauri ameeleza kuwa,  kulingana na utafiti uliofanyika umebaini uwepo wa hifadhi ya takribani tani milioni 5.5 ambazo zitachimbwa kwa muda wa miaka 24.

Kwa upande wa sekta ya ajira ndani ya mgodi huo, Shauri amesema mpaka sasa kampuni imeajiri wafanyakazi 290 , ambapo asilimia 43 ya wafanyakazi hao wanatoka katika vijiji vinavyozunguka mgodi na asilimia 52 ni wafanyakazi wanatoka nje ya vijiji vya mgodi huku asilimia 5 wanatoka nje ya nchi.

Kuhusu soko la madini, Shauri amesema, kwasasa  soko kuu la madini yanayozalishwa  na Lindi Jumbo lipo nchini India, hata hivyo kampuni inaendelea na jitihada mbalimbali za kutachakata  madini hayo kulingana na uhitaji wa masoko katika nchi mbalimbali kama vile China na Ujerumani.

Kutokana na maendeleo ya Sayansi na teknolojia madini kinywe yanatumika kutengeneza betrii za magari hususan kwenye magari yanayotumia mafuta, hutumika kwenye mikanda ya breki za magari, hutumika kulainisha  sehemu za mitambo yenye joto kali.

Pamoja na matumizi mengine, madini kinywe pia hutumika kutengenezea vikombe (Crucible) kwenye  viwanda vya chuma lakini pia hutumika kutengeneza paneli za umeme jua  hii ni
kutokana na sifa yake ya kuhimili joto kali.

#Vision2030:MadiniNiMaishaNaUtajiri
#MineralValueAddition
#GDP:10.1%FromMineraSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals