[Latest News]: Rais Samia Amkubali Dkt. Biteko Kuisimamia Sekta

Tarehe : Oct. 16, 2022, 10:19 a.m.
left

Ampa Kongole kwa kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko katika kuisimamia Sekta ya Madini.

Rais Samia amempongeza Dkt. Biteko leo Oktoba 16, 2022 wakati akiwasalimu wananchi wa Runzewe Jimbo la Bukombe mkoani Geita na kuzungumza nao masuala mbalimbali akiwa safarini kuelekea mkoani Kigoma.

"Ndio maana mnaona nawagusa wote nawabadilisha lakini Biteko yupo hapo katika Wizara ya Madini kwa sababu ninaye kijana anayefanya kazi nzuri na anaisaidia Tanzania," amesema Rais Samia.

Amesema, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 4 na sasa unachangia karibu asilimia 8 ya mchango wake kwa Taifa.

Vile vile, amemtaka kuhakikisha mchango wa Sekta ya Madini unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 ili iweze kuchangia zaidi katika Pato la Taifa.

Aidha, amemtaka kuongeza bidii katika kusimamia shughuli za kuisimamia Sekta kwa kuwa anao uwezo wa kutosha katika shughuli za madini.

Rais Samia amefanya ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Geita ambapo amezindua Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu kilichopo mkoani humo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals