[Latest News]: MKUTANO WA SABA WA KIMATAIFA SEKTA YA MADINI  KUFANYIKA NOVEMBA, 2026

Tarehe : Aug. 24, 2025, 11:17 a.m.
left

Yaelezwa Sababu ni kupisha maandalizi ya Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu

Dodoma

Wizara ya Madini imetangaza kusogeza mbele Mkutano wa Saba (7) wa  Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliokuwa  ufanyike mwezi Novemba 2025 na badala yake mkutano huo utafanyika tarehe 19 hadi 21 Novemba 2026, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar EsSalaam.

Taarifa iliyotelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng. Yahya Samamba imeleza  sababu za  kusogezwa kwa mkutano huo kuwa ni kupisha maandalizi ya Uchaguzi Mkuu  wa nchini uliopangwa kufanyika  mwishoni  mwa mwezi Oktoba, 2025.

‘’Wizara ya Madini inaomba radhi kwa wadau wote wa ndani na nje ya nchi waliokuwa wanatarajia kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini ambao ulipangwa kufanyika Novemba 2025,’’ imeeleza taarifa hiyo.

Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini unaofanyika kila mwaka tangu 2019 ukibebwa na kaulimbiu mbalimbali, hutumika kama jukwaa la kujadili kwa pamoja mstakabali wa Sekta ya Madini, kubadilishana ujuzi, maarifa na uzoefu pamoja na kuangazia fursa mpya zinazojitokeza katika Sekta ya Madini nchini.

Vilevile, mkutano huo hutumika kuimarisha mazingiraya uwekezaji, kuendelea kuvutia uwekezaji mpya kutoka ndani na nje ya nchi, wadau kupata fursa ya kujifunza Sera, Sheria  na mikakati  mipya ya Serikali na  kujadili kwa pamoja masuala ya kisheria na uchumi yanayohusiana na Sekta ya Madini.

Mbali na hayo,  kupitia  hafla ya  Usiku wa Madini ambayo huambatana na mkutano huo,  hutumika kutoa tuzo kwa wadau waliofanya vizuri katika Sekta ya Madini  kupitia vipengele mbalimbali ikiwa ni ishara ya kutambua  mchango wao kwa Sekta ya Madini nchini.

Aidha, mkutano huo huyakutanisha makundi mbalimbali wakiwemo mawaziri wa madini kutoka nchi nyingine za Afrika, watendaji wakuu wa kampuni kubwa za madini duniani waliowekeza nchini, watafiti,  mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa chini na nje ya tanzania, mashirika ya kimataifa.

Makundi mengine ambayo hushiriki mkutano huo ni pamoja na wachimbaji, wafanyabiashara wa madini, taasisi za fedha, vyuo vikuu na vya kati, taasisi za umma, taasisi binafsi zinazojishughulisha na  madini, viongozi mbalimbali kutoka wizara, taasisi za umma, mikoa na halmashauri ambazo shughuli za madini zinafanyika.

#Vision 2030:
Madini ni Maisha na Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals