[Latest Updates]: Mafanikio ya Utekelezaji Wa Bajeti ya Mwaka 2019/2020

Tarehe : March 25, 2020, 10:10 a.m.
left

Wizara ya Madini tarehe 23 na 24 Machi, 2020, ilikutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Jijini Dodoma ambapo iliwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa  Majukumu na Bajeti ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

 Akiwasilisha taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alibainisha baadhi ya mafanikio ya wizara kuwa ni pamoja na;

 • Katika kipindi cha nusu mwaka (Januari hadi Juni, 2019) kasi ya ukuaji wa uchumi katika Sekta ya Madini ulifikia asilimia 13.7 na kushika nafasi ya pili kitaifa ikitanguliwa na Sekta ya Ujenzi iliyokua kwa asilimia 16.5. Aidha, ukuaji wa Sekta ya Madini hadi kufika robo ya tatu ya Mwaka (Januari hadi Septemba, 2019) ulifikia asilimia 12.6 na kuendelea kushika nafasi ya pili kitaifa ikitanguliwa na Sekta ya Ujenzi iliyokua kwa asilimia 14.8. Ukuaji huu ulitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu, makaa ya mawe, na almasi kati ya madini mengine. Katika kipindi hicho, uzalishaji wa dhahabu uliongezeka hadi kilo 31,615 kutoka kilo 28,338 mwaka 2018. Uzalishaji wa makaa ya mawe uliongezeka hadi tani 517,986 kutoka tani 483,481 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Ukuaji huu umeifanya sekta ya kuwa ya pili katika kasi ya ukuaji kwa kipindi rejea ikitanguliwa na sekta ya Ujenzi iliyokua kwa asilimia 14.8.
 • Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa (GDP) umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka kutokana na ongezeko la kasi ya ukuaji wa sekta ikishindanishwa na sekta nyingine za kiuchumi. Katika kipindi cha nusu mwaka (Januari hadi Juni, 2019) mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa ulikuwa asilimia 5.1. Aidha, hadi kufika robo ya tatu ya Mwaka (Januari hadi Septemba, 2019) mchango wa Sekta hii ulikuwa asilimia 4.7.
 • Wizara ya Madini ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi 470,897,011,000.00 katika Mwaka wa Fedha 2019/2020. Hadi kufikia Februari, 2020 jumla ya Shilingi 319,025,339,704.73 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la makusanyo ya katika kipindi husika.
 • Kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha usimamizi wa biashara ya madini kumekuwa na ongezeko la mauzo ya madini katika masoko na vituo vilivyoanzishwa ambapo kilo 9,237.34 za dhahabu, karati 12,973.14, za almasi, kilo 20,099.17 za madini ya bati na kilo 514,683.28 za madini ya vito ziliuzwa na kuipatia Serikali mapato ya Shilingi 66,572,127,424.45 kutokana na mrabaha na tozo mbalimbali katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi 2019 hadi Januari, 2020. Aidha, Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania inaonyesha kuwa kwa mwaka ulioishia Novemba, 2019 mauzo ya dhahabu nchi za nje yalikuwa ni Dola za Marekani milioni 2,139.9 sawa na ongezeko la 41.9% kutoka mwaka uliopita. Mauzo hayo ni sawa na 51.4% (zaidi ya nusu) ya mauzo ya nje ya nchi ya bidhaa zisizo za asili.
 • Baada ya Wizara kufanya kaguzi za kimkakati za leseni za biashara ya madini katika maeneo ya Geita, Mara, Mwanza, Chunya, Kahama na Arusha kumekuwepo na ongezeko la leseni 308 kutoka leseni 696 za biashara ya madini kabla ukaguzi wa kimkakati hadi kufikia leseni 1,004. Ongezeko hili pia limechangiwa na kuimarika kwa utendaji wa Tume ya Madini.
 • Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2019 hadi Februari, 2020 Tume ya Madini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama imefanikiwa kukamata madini ya aina mbalimbali yenye thamani ya Dola za marekani 3,210,976.35 na Shilingi 1,556, 209,334.61 katika maeneo ya Tunduru, Kyerwa, Mwanza, Mirerani, Holili, Babati, Hai, Dodoma, Nzega na Kahama.
 • Maabara ya GST ilipata ITHIBATI ya kimataifa ya uchunguzi wa sampuli za dhahabu kwa njia ya tanuru kutoka shirika la SADCAS. Hii itasaidia sampuli zinazopimwa katika maabara zetu ziweze kuaminika kimataifa na kuruhusu upimaji wa sampuli kutoka nje ya nchi na kupunguza gharama za uchunguzi wa sampuli zetu nje ya nchi.
 • Tanzania ni moja ya nchi wanachama waanzilishi wa Umoja wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), umoja huu ulikuwa na makubaliano ya mashirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo Sekta ya Madini. ICGLR imekuwa ikitoa 118 mafunzo ambayo yamekuwa na mchango mkubwa kwa nchi wanachama katika kufahamu masuala yanayohusu madini ya 3Ts (Tin, Tungsten na Tantalum). Mafunzo haya yametoa nafasi kwa nchi wanachama kufuatilia shughuli za madini ya bati kwa vitendo (field practice). Hatua hii imeiwezesha Nchi yetu kukamilisha vigezo vilivyokubalika na ICGLR na kupata ithibati (certification) na hivyo kuweza kufanya biashara bila ya vikwazo vya ICGLR. Aidha, tangu kutolewa kwa cheti hicho mwezi Februari, 2020 hakuna usafirishaji wa madini ya bati nje ya nchi uliofanyika kutokana na mnunuzi mkuu na pekee wa madini hayo ambayo ni Kampuni ya Tanzaplus kusimama uendeshaji wa smelter tangu Agosti, 2019 kutokana na changamoto za kiuendeshaji. Mnunuzi huyo anatarajia kuanza shughuli hizo Machi, 2020.
 • Baada ya kuhamasishwa kuhusu uongezaji thamani madini, Wizara kupitia Tume ya Madini mpaka kufikia Machi, 2020 imetoa leseni mbili za uyeyushaji madini ya metali (smelters) zilizopo katika Wilaya za Mpwapwa na nyingine Kahama. Pia, Wizara kupitia Tume ya Madini imetoa leseni tatu za usafishaji madini (refinery) katika mkoa wa Dodoma, Geita na Mwanza. Viwanda hivyo vya uongezaji thamani madini vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kiwanda cha usafishaji madini kilichopo Dodoma kipo katika hatua za mwisho.

Akizungumzia Taarifa ya Masoko ya Madini alieleza kuwa,

 • Uanzishwaji na Uimarishwaji wa Masoko ya Madini Hadi kufikia Februari, 2020 jumla ya masoko 28 na vituo vidogo 28 vya ununuzi wa madini vimeanzishwa. Manufaa yaliyotokana na masoko hayo ni pamoja na kuongezeka kwa maduhuli ambapo kwa kipindi cha Machi, 2019 hadi Januari, 2020 jumla ya Shilingi 66,572,127,424.45 zilikusanywa kupitia masoko hayo. Aidha, uanzishwaji wa masoko umesababisha uwepo wa ajira za moja kwa moja ambapo jumla ya watu 165 wameajiriwa. Ajira hizo zinajumuisha watu 140 kwenye masoko ya madini na watu 25 kwenye vituo vidogo vya ununuzi wa madini.

Akitaja sababu za kufikiwa kwa Mafanikio hayo ya uendeshaji na Usimamizi wa Masoko Prof. Msanjila alisema;

Kufikiwa kwa malengo ya ukusanyaji wa maduhuli kwa kipindi husika kumetokana na juhudi zifuatazo:

 1. uwepo na usimamizi wa masoko ya madini pamoja na vituo vya ununuzi wa madini ambao umerahisisha biashara ya madini hususan kwa wachimbaji wadogo na hivyo kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki;
 2.  (ii) kuendelea kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini;
 3.  (iii) kuimarisha uboreshaji na usimamizi wa bei elekezi za madini ya vito kulingana na mwenendo wa masoko ya kimataifa. Mkakati huu umeiwezesha Tume kupata thamani halisi ya madini yanayozalishwa na hivyo kupata mapato stahiki;
 4.  (iv) kuendelea kutumia mfumo wa GePG ambao umerahisisha ulipaji wa tozo mbalimbali na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali;
 5. (v) utoaji wa leseni mbalimbali za utafutaji, uchimbaji mdogo, uchimbaji wa kati, uchenjuaji, usafishaji, uyeyushaji na biashara ya madini; na (vi) kuendelea kutoa elimu ya Sheria ya Madini pamoja na kuendesha mafunzo ya mara kwa mara katika maeneo ya wachimbaji wadogo ili kujenga uelewa wa Sheria hiyo na kulipa kodi stahiki kwa Serikali

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals