[Latest Updates]: Serikali kuifutia leseni Kampuni ya uchimbaji almasi ya El Hilal ikishindwa kulipa deni

Tarehe : April 28, 2018, 12:26 p.m.
left

Serikali imetoa mwezi mmoja kwa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Almasi ya El Hilal kulipa zaidi ya Shilingi bilioni 3.4 ikiwa ni ada ya mwaka pamoja na mrabaha wa mauzo ya almasi nchini na endapo itashindwa kufanya hivyo itafutiwa leseni yake.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila,( wa pili kushoto( katikati)akionyeshwa sehemu ya mitambo ya Mgodi wa El Hilal unaochimba Madini ya Almasi.[/caption]

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua migodi ya uzalishaji almas ya kampuni za Wiliamson Diamond na El Hilal zilizopo eneo la Mwadui mkoani Shinyanga,Februari 21, 2018.

Prof. Msanjila alisema mgodi wa El Hilal unamiliki leseni kubwa ya uchimbaji wa madini ya almas,iliyotolewa mwaka 2010 na unadaiwa ada ya mwaka ( annual rent) Dola za Kimarekani 1,447,360 sawa na shilingi bilioni 3.1 ambazo hazijalipwa kwa kipindi cha miaka 6, kuanzia 2012/13 hadi 2017/18.

Vilevile aliweka wazi kuwa kampuni hiyo pia inadaiwa zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 294.2 ikiwa ni mrabaha pamoja na adhabu yake iliyotokana na mauzo ya ndani ya almasi yaliyofanyika
kwa kipindi cha miaka tatu kuanzia 2011 hadi 2013.

“ Haiwezekani kampuni ikawa inafanya biashara ndani ya kipindi chote hicho halafu hailipi mapato ya Serikali, Sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 iko wazi inaelekeza hatua za kuchukua kwa vitendo kama hivyo, sasa tumewapa muda na sheriaitachukua mkondo wake”, alisema Msanjila.

Aidha aliitaka kampuni hiyo kufanya shughuli zake kwa kuziangatia Sheria na Kanuni za uchimbaji madini, na pia katika kutoa ajira kwa wafanyakazi wake na kwamba sheria na kanuni za madini zinapaswa kufuatwa hata kama ni mwekezaji mzawa.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila,( wa tatu kushoto) akionywesha baadhi ya mitambo ya Mgodi wa uchimbaji almasi ya El Hilal iliyopo Mwadui, Shinyanga.[/caption]

Sambamba na hilo,Msanjila ilizitaka kampuni za uchimbaji zinazoendeshwa na wawekezaji wa nje kuwa na akaunti za fedha hapa nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo kampuni nyingi akaunti zake zipo nje ya Tanzania.

Msanjila pia aliwataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, juhudi na maarifa na bila kumpendelea mtu yeyote wakati wakitekeleza
majukumu yao.

Vilevile aliwataka kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali katika madini yanayopatikana kwenye maeneo yao, akitolea mfano wa Madini ya Ujenzi kuwa yamesahaulika kabisa katika makusanyo.

Aliendelea kuwakumbusha Makamishna hao kuendelea kutoa elimu sahihi kwa wachimbaji na wadau wote wa madini katika maeneo yao juu ya marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 pamoja na kanuni zake.

Imeandaliwa na:

Zuena Msuya, Shinyanga

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals