[Latest News]: TGC Yafungua Vituo Kutangaza Fursa Zailizopo Kwenye Sekta ya Madini ya Vito

Tarehe : Nov. 7, 2025, 4:04 p.m.
left

Arusha

Katika juhudi za kuendeleza  kutangaza fursa mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo wa uongezaji thaman madini ya vito na metali za thamani, Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kimefungua vituo maalum vya kutangaza fursa zilizopo kwenye mnyororo wa uongezaji thamani madini nchini katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) na katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Hayo yamebainishwa leo Novemba 7, 2025 na Mkuu wa Kituo  hicho Mha. Ally  Maganga wakati akielezea namna vituo hivyo vitakavyotangaza fursa mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo mzima wa thamani madini hususan kwa wageni wa ndani na nje ya nchi.

Akielezea kuhusu faida zitakazopatikana kupitia vituo hivyo  Mha. Maganga  amesema kuwa, lengo kubwa la kufungua vituo hivyo ni kutangaza, kuelimisha, kuhamasisha, kukuza uelewa kwa jamii kuhusu shughuli zinazofanywa na TGC. 

Sambamba na fursa za kimataifa, pia vituo hivyo vitafungua fursa za upatikanaji wa ajira na kuongeza  shughuli za ujasiriamali kwa vijana mbalimbali wenye ujuzi katika uongezaji thaman madini  hususan katika viwanda vya usonara.

Mha. Maganga amefafanua kuwa, mbali na fursa hizo, vituo hivyo  vitahamasisha na kuvutia uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa madini itakayosaidia uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata madini ya vito na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na rasilimali madini kama vile herein, pete, shanga , vinyago , mikufu na tuzo.

Akielezea kuhusu Utalii wa madini Mha. Maganga ameeleza kuwa,  faida nyingine  ni kukuza utalii wa madini   kupitia watalii wanatoka na kuingia nchini  kupitia kiwanja cha KIA na wageni watakaoshiriki mikutano ya kitaifa na kimataifa kupitia ukumbi wa  AICC.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Kati wa Madini (Broker) Jeremiah Kituyo ameipongeza TGC kwa kupanua wigo wa fursa za kibiashara utakaohamasisha ushirikiano mzuri kati ya Sekta Binafsi na Serikali hasa kwenye mnyororo wa uongezaji thaman madini ya vito na metali za thamani (precious metals) kama Sera ya Madini ya Mwaka 2009 inavyoelekeza.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals