[Latest Updates]: Waziri Dkt.Biteko atanguliza mbele ajira kwa Watanzania

Tarehe : Feb. 14, 2022, 12:43 p.m.
left

Waziri wa Madini, Dkt.Doto Biteko amesema Kampuni ya Kabanga Nickel ambayo ni mbia wa Serikali kupitia Kampuni ya Tembo Nickel itatoa fursa zaidi za ajira kwa Watanzania hususan wakazi wa wilaya ya Ngara na mkoa wa Kagera ili washiriki katika  shughuli mbalimbali za uzalishaji ndani ya kampuni.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 14, 2022 katika kikao na wawekezaji kutoka Kabanga Nickel wanaochimba madini ya Nickel kilichofanyika jijini Dodoma.

Amewataka, Watanzania wenye sifa na uzoefu katika fani mbalimbali kujitokeza kuomba nafasi zinazotangazwa na Kampuni ya Kabanga Nickel ili wapate fursa zaidi na kukuza maendeleo.

Aidha, Dkt. Biteko amesisitiza kufuata Sheria za Madini hususan ushirikishwaji wa wazawa kwenye masuala ya manunuzi, ajira na uhawilishaji wa ujuzi (local content).

Pia, Dkt.Biteko amesisitiza Kampuni ya Kabanga kuhakikisha kwamba uchimbaji wa madini unazingatia masuala ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii inayozunguka mgodi (CSR).

Amesema, Serikali imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji katika Sekta ya Madini ili waweze kufanya shughuli za uchimbaji madini kuwa zenye tija kwa nchi na wawekezaji wenyewe kwa kuondoa vikwazo mbalimbali.

Kwa upande wake, Meneja Mkazi wa Tembo Nickel, Benedict Busunzu amesema ajira nyingi zimeanza kutolewa ili watanzania wenye sifa waweze kupata nafasi. Amesema, fursa zipo wazi na matangazo ya nafasi mbalimbali zimeanza kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari.

Kwa upande mwingine, Dkt. Biteko  amekutana na Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA) kujadili mambo mbalimbali yanayohusu uzalishaji huo.

Wengine, waliohudhulia kikao hicho ni Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga,  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Dkt.Mussa Budeba Kamishna wa Tume ya Madini,  Prof.Abdulkarim Mruma, na Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara na Tume ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals