[Latest Updates]: Wachimbaji madini kulipa kodi na tozo mbalimbali

Tarehe : Dec. 28, 2017, 9:46 a.m.
left

Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini wametakiwa kutambua wajibu wao wa kulipa Tozo na Kodi mbalimbali Serikalini kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye eneo la machimbo ya Dhahabu la Buhemba. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.[/caption]

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye eneo la machimbo ya Dhahabu la Buhemba Wilayani Butiama, Mkoani Mara.

Alisema Serikali haina kikwazo na wachimbaji wadogo na inafanya jitihada za kuwasaidia kuwa na uchimbaji wenye tija hata hivyo alisema wanapaswa kutambua wajibu wao wa kulipa kodi ambayo itawanufaisha wao kama wachimbaji lakini pia Jamii inayozunguka maeneo yenye migodi na Taifa kwa ujumla.

Baadhi ya Wachimbaji kwenye Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).[/caption]

Aliongeza kuwa Rasilimali Madini ni kwa ajili ya Watanzania wote na kwamba kila Mwananchi anayo haki ya kunufaika nayo kwa namna moja ama nyingine mojawapo ikiwa ni manufaa yatokanayo na kodi zinazolipwa kutokana na shughuli za uchimbaji.

“Serikali inahitaji ipate kodi yake kwani madini yanapaswa kuwaneemesha Watanzania wote. Mtakavyolipa kodi, fedha husika zitatumika kuwaletea na kuwaboreshea huduma mbalimbali ikiwemo elimu, afya na miundombinu mbalimbali,” alibainisha Naibu Waziri Nyongo.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na baadhi ya Wachimbaji kwenye Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba.[/caption]

Aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuwarasimisha Wachimbaji wa Madini kwa kuwapatia Leseni za Uchimbaji ili wachimbe kwa kufuata utaratibu unaotakiwa kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya Mwaka 2017.

Alisema Sheria hiyo vilevile inazungumzia suala la uundaji wa Tume ya Madini yenye jukumu la kusimamia shughuli zote za madini ikiwemo utoaji wa leseni.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi wakati wa ziara yake kwenye eneo la machimbo ya dhahabu la Buhemba, Wilayani Butiama, Mkoani Mara.[/caption]

Aliwaasa wachimbaji kote nchini kujiunga katika vikundi ili kupatiwa leseni na alibainisha kwamba kati ya Mwezi Januari na Februari, 2018, Tume hiyo itakuwa imeanza kazi rasmi.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo alibainisha kwamba mbali na utoaji wa huduma bora kwa wachimbaji wa madini na wananchi kwa ujumla, Serikali inao wajibu wa kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili kuwa na uchimbaji wenye tija.

Aliziagiza Ofisi za Madini kote Nchini kwa kushirikiana na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ikiwemo Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuhakikisha Wachimbaji hususan wadogo wanapatiwa elimu ya mara kwa mara ya uboreshaji wa shughuli zao.

Imeandaliwa na:

Mohamed Saif,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals