[Latest Updates]: Madini Mkakati Yajadiliwa Mkutano wa 9 EITI

Tarehe : June 15, 2023, 12:56 p.m.
left

Dakar, Senegal

Mkutano wa Kimataifa wa Asasi ya Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji _*(EITI - Extractive Industry Transparency Initiative)*_ uliofanyika Jijini Dakar nchini Senegal kuanzia tarehe 13 -14 Juni 2023 umejadili fursa mbalimbali kwenye Sekta ya Madini ikiwemo namna nchi zenye utajiri wa Madini Mkakati zinavyoweza kuzalisha Madini hayo kwa kuzingatia vigezo vya Uwazi na Uwajibikaji ili kuhakikisha kuwa Madini hayo yanawanufaisha wananchi wa maeneo yanapozalishwa na kuchangia katika kuinua uchumi wa mataifa husika.

Akichangia hoja katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa alisema Tanzania ina aina nyingi za Madini mkakati yakiwemo *_Nikeli, Graphite (Kinywe), Rare Earth Elements, Cobalt, Lithium, Manganese, Vanadium, Niobium, Titanium, Tin, na Copper (Shaba)._* 

Aliongeza kuwa, Madini hayo yanahitajika kwa wingi duniani kwa sasa na hivyo kinachohitajika zaidi ni ushirikiano _*(Partnerships)*_ kati ya Serikali na wawekezaji mahiri kwenye masuala ya utafiti wa kina, uchimbaji wa kisasa, na uchakataji wa bidhaa za ndani na kuyaongeza thamani Madini ndani ya nchi suala ambalo litaongeza tija na kutoa fursa za ajira kwa wazawa na kukuza biashara ya bidhaa za Madini yaliyoongezwa thamani kwa walaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi. 

Aidha, katika mkutano huo, mada mbalimbali zilijadiliwa kwa siku mbili ikiwa ni pamoja na masuala ya vipaumbele katika Uwajibikaji na Uwekaji wazi kumbukumbu za uzalishaji na biashara ya Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia katika kipindi cha miaka kumi ijayo; uwekaji wazi Mikataba kati ya Serikali na wawekezaji; uwekaji wazi takwimu za wenye hisa katika kampuni za uwekezaji; sambamba na kujadili mbinu za kukabiliana na rushwa na ufisadi katika Sekta za Madini, mafuta na Gesi Asilia.

Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na washiriki kutoka nchi zipatazo 90 ulihitimishwa Juni 14, 2023.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals