[Latest Updates]: Mbibo Afungua Mafunzo ya Ndani ya Utunzaji Nyaraka za Serikali

Tarehe : Feb. 9, 2022, 4:53 p.m.
left

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amefungua Mafunzo ya ndani kuhusu utunzaji wa Nyaraka, Uzingatiaji wa Kanuni katika kusimamia mwenendo wa Mafaili, Uandishi wa Nyaraka na Changamoto katika upatikanaji wa Majarada.

Mbibo amesema kumbukumbu katika taasisi au wizara yoyote ndiyo injini ya sehemu husika ambapo amewataka watumishi wote hususan watunza kumbukumbu kuhakikisha wanatunza nyaraka kwa uangalifu ili kuweza kufikia malengo ya Serikali.

“Naomba nitumie fursa hii kuwapongeza Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kwa kuandaa mafunzo haya ya ndani ili kuwajengea uwezo na kuwaongezea ufanisi wa kazi watumishi wanaohusika na utunzaji wa kumbukumbu pamoja na nyaraka mbalimbali za wizara.

Amesema Mafunzo hayo ni muhimu kuliko mafunzo ya shuleni ambayo hufundishwa zaidi nadhalia kuliko vitendo kama mafunzo hayo ambayo washiriki wanafundishwa kazi halisi zinazo wahusu wao.

Aidha, Mbibo ameongeza kuwa, Sheria ya utunzaji wa Nyaraka unaenda sambamba na utunza wa Siri za Serikali ambapo amewataka watunza kumbukumbu kuhakikisha wanakuwa waadilifu katika utendaji kazi wao na kuwataka kulinda Siri za Serikali, sio za kwenye makaratasi pekee ila mpaka Siri za mioyoni mwao.

Pamoja na mambo mengine, Mbibo amesema Sekta ya Madini inahitaji watumishi wenye uadilifu, uzalendo na wenye moyo wa kutunza kumbukumbu.

“Sekta ya Madini ni Sekta nyeti hiyo watumishi wa sekta hii tuwe waadilifu katika utendaji kazi wetu na pia tufuate Sheria na Taratibu zilizopo na ukizingati sekta hii ndiyo inayoongoza kuuza bidhaa zake nje ya nchi ambapo asilimia 50% ya bidhaa zote zinazouzwa nje ya nchi zanatokana na madini,” amesema Mbibo.

Sambamba na hayo Mbibo ametoa rai kwa Idara ya Utawara na Rasilimali Watu ambao wanahusika na usimamizi wa utunzaji wa kumbukumbu kuwa mfano wa utunzaji bora wa nyaraka na kumbukumbu za serikali.

Vile vile Mbibo ameelekeza kwamba, Masijala ziwe na watumishi wenye sifa na uadilifu, wawe na uwezo wa kusimamia vizuri vifaa vinavyotunza kumbukumbu za Siri ili zisiwafikie watu wasiohusika, Nyaraka za Siri zisidurufiwe, kutokufungua mafailli mengi ya muda, maafisa wasikae na mafaili kwa zaidi ya siku tano, Masijala isitumike kuhifadhi vitu vingine zaidi ya nyaraka na computa zote za masijala ziwekewe antivairas.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals