Tarehe : March 29, 2025, 11:08 a.m.
Dodoma
Baadhi ya Watumishi Wanawake Wizara ya Madini Machi 28, 2025 waliwawakilisha wenzao kutoa msaada kwa wahitaji waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Misaada iliyotolewa ni pamoja na Bima ya Afya kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa watoto Watatu (3) waliolazwa katika hospitali hiyo, vifaa
mbalimbali kwa watoto njiti ikiwemo sabuni, mafuta na mahitaji mengine ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma kuelekea Sikukuu za Eid na Pasaka.
Akizungumza katika tukio hilo, Afisa Ustawi Mwandamizi hospitali hiyo Elvira Mutagabwa, aliwashukuru watumishi hao kwa moyo waliouonesha wa kujali wenye mahitaji na kueleza kwamba, kitengo hicho kinazo changamoto nyingi kutokana na idadi ya wanaohitaji misaada ya matibabu na hivyo kutoa wito kwa jamii kuona umuhimu kusaidia wenye mahitaji.
Akizungumza kwa niaba ya wawakilishi wa watumishi wanawake Wizara ya Madini, Nuru Kiterebu alisema watumishi hao walifika ikiwa ni sehemu ya kufanya matendo ya huruma katika msimu huu wa kuelekea Sikukuu za Eid na Pasaka baada ya kupata taarifa kuhusu uwepo uhitaji wa huduma za matibabu.
" Huu ni mwanzo tukijaaliwa wakati mwingine tutaendelea kusaidia watoto wengine," alisema Kiterebu.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.