[Latest Updates]: Malawi Yashangazwa na Uwekezaji Mkubwa Geita Gold Mining

Tarehe : Sept. 25, 2025, 11:16 a.m.
left

Geita

Ujumbe maalum kutoka Serikali ya Malawi umeonesha kushangazwa na kuvutiwa na kiwango kikubwa cha uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika sekta ya uchimbaji wa madini ya dhahabu mkoani Geita.

Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo ya Biashara za Vikundi nchini Malawi,  Zizwan Khonje, ambaye amesema kuwa uwekezaji huo si tu unadhihirisha uwezo mkubwa wa kampuni hiyo, bali pia unaonesha kuwa Tanzania ni sehemu salama na bora kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

“Tumefurahishwa sana na kile tulichokiona hapa Geita. GGML imewekeza kwa kiwango kikubwa sana katika teknolojia, usalama, na maendeleo ya kijamii. Hili ni jambo la kujivunia, na ni mfano mzuri tunaopaswa kuiga nchini Malawi,” amesema Khonje mara baada ya kutembelea mgodi huo.

Khonje ametumia fursa hiyo kuipongeza GGML kwa namna inavyoendesha shughuli zake kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia maslahi ya jamii inayozunguka mgodi huo. Aidha, ameisifu Wizara ya Madini ya Tanzania kwa usimamizi thabiti unaoleta mafanikio ya kweli katika sekta hiyo nyeti.

“Tumekuja kujifunza na kuona namna nchi jirani zinavyofanikiwa katika sekta ya madini. Ziara hii imetufungua macho kuona kuwa kuna mifumo bora ya usimamizi, uwazi na ushirikishwaji wa jamii, ambayo sisi Malawi tunaweza kuitekeleza kwa mazingira yetu,” ameongeza.

Katika ziara hiyo, ujumbe huo kutoka Malawi pia umetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na kukaribishwa rasmi na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mohamed Gombati ambapo amesema kuwa Tanzania na Malawi zimekuwa na uhusiano wa kihistoria wa muda mrefu, na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo unaendelea kuimarika katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, elimu na rasilimali madini.

“Tanzania na Malawi ni mataifa jirani yanayoshirikiana kwa karibu sana. Tunafarijika kuona kuwa mmeamua kutembelea Geita ili kujifunza. Tunaamini haya ni matunda ya ushirikiano wetu wa muda mrefu, na tunaendelea kuwakaribisha wakati wowote,” amesema Gombati.

Ujumbe huo pia umepata fursa ya kujifunza kuhusu mchango wa GGML katika maendeleo ya jamii, ikiwemo miradi ya afya, elimu, maji safi na uwezeshaji wa wajasiriamali kupitia mfumo wa uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Malawi katika kuimarisha sekta yake ya madini kwa kujifunza kutoka kwa nchi jirani zilizoendelea zaidi katika sekta hiyo, kwa lengo la kuboresha sera, mifumo ya usimamizi na kuvutia wawekezaji wa kimataifa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals