Tarehe : March 8, 2026, 10:59 a.m.
Senyamule awataka Wanawake Kuongeza Bidii kwenye Uthubutu
Kongwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimaifa ya Wanawake Duniani Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wanawake nchini kuitumia siku hiyo kutathmini hatua mbalimbali zilizopigwa za usawa wa kijinsia
huku akiwasisitiza kuongeza bidii kwenye uthubutu.
Ameongeza kwa kuwataka kutumia siku hiyo kuhamasisha kuhusu fursa za haki za uchumi na kuwaunga mkono wanawake walioonesha njia.
Katika Maadhimisho hayo Watumishi Wanawake Wizara ya Madini wameungana na wenzao kutoka Mkoa wa Dodoma ambapo takribani wanawake elfu Sita kutoka maeneo
mbalimbali zikiwemo Wizara, taasisi na makundi mbalimbali wameshiriki kuadhimisha ngazi ya Mkoa mkoani humo.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka.
Mwaka huu Maadhimisho hayo yamebebwa na kaulimbiu isemayo
Haki kwa Wanawake na Wasichana: Msingi wa Maendeleo Jumuishi kufikia Dira 2050
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.