Tarehe : March 12, 2025, 1:23 a.m.
Madini Mkakati ‘’Critical Minerals”
ARUSHA
Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga leo tarehe 12 Machi, 2025 ameshiriki kikao cha utangulizi cha Bodi ya Kimataifa ya EITI kilichojadili masuala ya Madini Mkakati.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka kwenye umoja wa nchi wanachama wa Kimataifa EITI.
Lengo la kikao hicho ni kuzindua utafiti kuhusu Madini Mkakati na hatari za Rushwa zinazoweza kujitokeza katika uvunaji wa Madini hayo.
Aidha,kikao hicho kimejadili suluhisho la kisera ili kulinda Madini Mkakati kwa lengo la kuwezesha mhamo wa Nishati (Energy transition)
Akizungumzia katika kikao hicho Dkt. Mwanga alilisitiza kuwa kutokana na uhitaji wa Madini hayo muhimu duniani sambamba na ukuaji wa teknolojia ni vyema kuwepo na mkakati wa uvunaji wa madini hayo muhimu Barani Afrika ambapo mkakati huo utasadia kwa nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Afrika kutengeneza mikakati yao inayoendana na mkakati mkubwa wa Dunia.
Amesema, wizara kupitia geological survey of Tanzania (GST) imejipanga kikamilifu kufanya tafiti mbalimbali za madini ikiwemo kutoa ushauri elekezi kupitia wataalumu wake, kudhibiti na kuzuia mianya yote ya rushwa.
Aidha,Kikao hicho kilihudhuriwa na CPA. Ludovick Utouh mwenyekiti wa Kamati ya TEITI pamoja na Katibu Mtendaji wa TEITI Bi. Mariam Mgaya.
Picha na matukio mbalimbali katika kikao hicho:
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.