[Latest Updates]: Madini Ujenzi, Viwandani Yenye Thamani Zaidi ya Trilioni Moja  Yazalishwa

Tarehe : Nov. 28, 2025, 11:27 a.m.
left

Ni madini muhimu kwenye Sekta ya Ujenzi

Dar es salaam

Imeelezwa kwamba, katika kipindi cha mwaka mmoja wa Fedha 2024/25 Madini Ujenzi na Viwandani yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni  Moja yalizalishwa.

Hayo yalielezwa Novemba 27, 2025 na Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa wakati wa utoaji Tuzo za Ujenzi na Miundombinu za Afrika Mashiriki zilizotolewa Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Steven  Kiruswa alisema kuwa, kutokana na kukua na kuendelea kwa sekta ya ujenzi nchini hususan kwenye ujenzi wa miundombinu na ukuaji wa sekta ya viwanda  kimezalishwa kiasi hicho cha fedha kupitia wachimbaji wa madini hayo.

Dkt. Kiruswa aliongeza kuwa, kwa kipindi kirefu mchango wa madini ya viwanda na ujenzi yamekuwa na uwanja mpana kwenye kuchangia uchumi wa Taifa ikiwa pamoja na kutoa ajira kwa jamii, kuunganisha mnyororo wa thamani madini  kupitia biashara na wawekezaji wa ndani kuanzia ngazi wilaya mpaka Taifa.

Dkt.Kiruswa alifafanua kuwa Tanzania itaendelea kutumia  malighafi zake za  ndani kama vile mchanga, kokoto, chokaa, gypsum, kaolini,  mawe ya naksi  na saruji ili kupunguza gharama , kuharakisha miradi na kuiwezesha sekta binafsi kwenye mnyororo wa uchumi endelevu.

Sambamba na hayo Dkt.Kiruswa  aliwapongeza Chemba ya Sekta ya Ujenzi na Miundombinu Tanzania kwa kuandaa hafla ya Tuzo za Ujenzi na Miundombinu Afrika Mashariki, na kueleza  itakuwa chachu ya  kuongeza nguvu katika uzalishaji, uendelezaji na kuifungamanisha na sekta nyingine za kiuchumi.

Pamoja na mambo mengine Dkt.Kiruswa alitumia jukwaa hilo kuwaomba washiriki wa hafla hiyo kuwaasa vijana wa kitanzania kuipenda na kuilinda miradi ya ujenzi na miundombinu ambayo inajengwa kwa gharama kubwa. 

#MadiniNiMaishaNaUtajiri
#InvestInTanzaniaMiningSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals