[Latest Updates]: ESG kuwa Kipaumbele kwa Watumishi Wizara ya Madini na Taasisi zake

Tarehe : Feb. 27, 2026, 3:27 p.m.
left

Kuweka matumizi nishati Safi.
Kupunguza uzalishaji hewa ya ukaa
Kuhakikisha Usalama Kazini.
Uwazi wa taarifa za kifedha.

Dodoma

Watumishi wa Wizara ya Madini na taasisi zake wametakiwa kuzingatia viwango vya Kijamii, Mazingira na Utawala(ESG) katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuimarisha uwajibikaji, uendelevu na utawala bora katika Sekta ya Madini nchini.

Wito huo umetolewa leo Februari 27, 2026 na Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga  wakati akifunga mafunzo maalum yaliyolenga kuwajengea uwezo watumishi kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira , kuheshimu masuala ya kijamii na kuzingatia misingi ya uwazi na maadili katika utendaji kazi.

Dkt.Mwanga amesema kuwa, utekelezaji madhubuti wa kanuni za ESG utasaidia kuongeza imani ya wawekezaji , kulinda maslahi ya jamii zinazozunguka maeneo ya migodi na kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. 

Dkt.Mwanga amefafanua kuwa mojawapo ya kigezo cha uwekezaji ni suala la utunzaji wa mazingira kwa jamii hivyo  mafunzo haya yamewapa uelewa mpana kuhusu umuhimu wa tathimini za athari za mazingira , ushirikishwaji wa wadau pamoja na kuzingatia misingi ya maadili na uwajibikaji katika maamuzi ya kiutendaji.

Ameeleza kuwa, kwa kuzingatia viwango vya ESG mafunzo haya yanakuwa sehemu ya mkakati wa kuiwezesha sekta ya madini kuchangia kikamilifu maendeleo ya uchumi wa taifa kwa njia endelevu inayokubalika kimataifa.

Akizungumza kwa niaba ya waandaaji wa mafunzo hayo, Mratibu wa Mafunzo ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini CPA. Pili Kamali amesema kuwa moja ya malengo ya mafunzo ni kuhakikisha watumishi wanaandaa na kuwasilisha taarifa za fedha kwa kuzingatia misingi ya ESG  unasaidia kuongeza uwazi , uwajibikaji na uaminifu katika usimamizi wa rasilimali madini.

Kamali amefafanua kuwa  uandaaji wa taarifa za fedha unahusisha misingi ya ESG hususan katika kuzingatia athari za mazingira, kijamii na kiutawala kwa kufuata maelekezo ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi(NBAA).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals