Tarehe : Feb. 12, 2026, 9:32 p.m.
Asisitiza Miradi kuchangia Ustawi wa Jamii
Aomba ushirikiano utafiti wa kina kutoka asilimia 16 ya sasa
Chemba waomba kuharakishwa mikachato ya kiuwekezaji
Cape Town, Afrika Kusini
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amewapongeza Wanachama wa Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) kwa mchango wao katika mafanikio na Maendeleo ya Sekta ya Madini nchini.
Akizungumza Februari 11 jijini Cape Town katika hafla fupi iliyoandaliwa na TCM kwa ufadhili wa kampuni ya Alistair, ALN na Benki ya NMB, Waziri Mavunde alisema mafanikio ya sekta hiyo katika pato la Taifa, ajira na mapato ya fedha za kigeni hayawezi kutenganishwa na umoja huo na kwamba, yamechangiwa na ushirikiano imara uliopo kati ya Serikali na wadau.
Akitaja mafanikio na mwelekeo wa Sekta hiyo, Waziri Mavunde alisema Serikali inatarajia kusaini mikataba 13 ya uwekezaji katika miradi mikubwa ya madini, ikiwemo mradi wa uchimbaji na uchakataji wa madini ya niobium wenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1, ambao utaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa madini hayo duniani nyuma ya Canada na Brazil.
Kutokana na mafanikio hayo, alihimiza kuendelezwa ushirikiano wa karibu huku akisisitiza uwazi, kufanya kazi kama timu moja na kuhakikisha uwekezaji katika sekta ya madini unaleta ustawi wa pamoja kwa watanzania na ulenge kuifanya sekta ya madini kuwa kitovu cha uchumi wa taifa.
‘’ Lakini niendelee kuwaomba tuendelee kushirikiana kupitia vision 2030 Madini ni Maisha na Utajiri ikiwezekana tuvuke asilimia 16 ya sasa,’’ alisema Mavunde.
Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Botswana na Lesotho Mhe. James Bwana, alizipongeza kampuni za madini zilizowekeza Tanzania na kueleza kwamba mlango wa ushirikiano bado uko wazi kwa wageni kuendelea kuwekeza. Aidha, amempongeza Mwenyekiti wa Tume ya madini Dkt, Janeth Lekashingo kwa namna alivyoiwakilisha Tanzania kuchangia kwenye midahalo mbalimbali katika kongamano la Mining Indaba.
Naye, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi Mhandisi Philbert Rweymamu, alimpongeza Mhe. Mavunde kwa kuchaguliwa tena kuingoza Wizara ya madini na mchango wake kwenye usimamizi wa sekta uliopeleka kuongezeka kwa mchango wa sekta ya Madini kwenye pato la taifa, ukuaji wa sekta ya fedha za kigeni.
Mhandisi Rweyemamu aliomba Serikali kuongeza ushirikiano katika maeneo mbali mbali kama vile kanuni za matumizi ya fedha za kigeni nchini, kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini, na michakato mbali mbali ambayo yataharakisha miradi kuendelea na kuwezesha mapokeo ya teknolojia ambazo hazipo nchini.
Pia, Rweyemamu aliomba kurejeshwa kwa utaratibu wa wizara na chemba ya migodi Tanzania kukutana mara kwa mara kwaajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu Sekta ya Madini nchini ili kuharakisha maendeleo.
Chemba ya migodi inaundwa na wachama kutoka kampuni kubwa na kati za madini, watoa huduma migodini na wanawake waongeza thamani madini.
#Mining4Development
#Vision2030
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.