[Latest Updates]: Waziri Mavunde, Watalaam Wajadili Mikakati Kuongeza Mapato ya Serikali, Manufaa Zaidi ya Sekta

Tarehe : Feb. 16, 2026, 10:55 a.m.
left

 Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony  Mavunde leo Februari 16, 2026 ameongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Madini, Taasisi na wataalam kujadili  mikakati ya namna bora ya kuongeza mapato ya Serikali yatokanayo na rasilimali madini kwa lengo la kuongeza  mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa, uchumi, ustawi wa jamii na kuwezesha miradi mingine ya maendeleo.

Aidha, kikao hicho kimejadili mikakati madhubuti ya kuendeleza Sekta ya madini  ili kuongeza tija zaidi na manufaa ya rasilimali  madini kwa  kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,  Dira ya Madini 2030 inayolenga kufanya tafiti za kina za madini  angalau kufikia asilimia 50 kutoka 16 ya sasa na Ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) za Mwaka 2025-30 katika Sekta ya Madini.

Mbali na wataalam hao, kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals