[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa-Usalama Mahala Pa Kazi Iwe Kipaumbele Migodini

Tarehe : July 7, 2022, 10:37 p.m.
left

Imeelezwa kuwa, usalama mahala pa kazi ni jambo muhimu ambalo linapaswa kuzingatiwa na wachimbaji wote wa madini nchini akiwemo mwajiri pamoja na waajiriwa, wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa

Hayo, ameyabainishwa na Dkt. Kiruswa baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji na uchenjuaji madini ya dhahabu wa Maweni Gold Mine uliopo katika kijiji cha Maweni mkoani Manyara

Dkt. Kiruswa amesema usalama katika shughuli za uchimbaji madini ni suala muhimu kuliko hata madini yanayochimbwa katika eneo husika ambapo amewataka waajiri na waajiriwa kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anajilinda na kuwalinda wengine

Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amewapongeza wawekezaji katika mgodi huo na kuwataka kuzingatia Sheria za Madini ikiwemo kulipa kodi na tozo mbalimbali za serikali

Naye, Kamshna wa Madini Dkt. Abdulrahiman Mwanga amemtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Manyara Mhandisi Ernest Sanka kutoa semina na mafunzo mbalimbali kuhusu elimu ya usalama mahala pa kazi ili wafanye shughuli zao kwa usalama

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanga ameutaka uongozi wa kampuni ya Maweni Gold mine Ltd kuhakikisha unajenga mahusiano mazuri na jamii iyozunguka eneo wanalofanyia shughuli za madini

Naye, Meneja wa Maweni Gold Mine Ltd Emmanueli Maguzu amesema mgodi wao umefunguliwa rasmi tarehe 4 Julai na unatarajiwa kuzalisha kilo moja na nusu za dhahabu kwa mwezi

Pia, Maguzu amesema kuwa, kwa sasa mgodi huo umeajiri wafanyakazi 20 upande wa uchenjuaji, wapishi wawili pamoja na walinzi 10 ambapo wanategemea kuajiri wafanyakazi wengi zaidi watakapoanza shughuli za uchimbaji ambapo kwa sasa wameanza shughuli za uchenjuaji pekee

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals