[Latest Updates]: Kampuni ya Perseus Yatangaza Kuanza Ujenzi wa Mgodi wa Dhahabu Nyanzaga Wilayani Sengerema

Tarehe : April 28, 2025, 9:20 p.m.
left

 Mradi wa ujenzi wa mgodi kugharimu Trillioni 1.4

 Dhahabu ya kwanza kuanza kuzalishwa robo ya kwanza ya Mwaka 2027

Rais Samia apongezwa kwa mazingira bora ya uwekezaji

Mgodi kuzalisha Ajira na mapato kwa serikali

Kampuni ya Perseus ya Nchini Australia yatoa tangazo rasmi la kuanza ujenzi wa mgodi wa dhahabu wa Nyanzaga uliopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Taarifa hiyo iliyotolewa leo tarehe 28 Aprili, 2025 imeeleza kuwa takribani kiasi cha Shilingi Trilioni 1.4 sawa na Dola za Kimarekani Milioni 523 (pamoja na dharura) zitawekezwa kujenga mgodi mkubwa unaotarajiwa kuzalisha dhahabu ya kwanza katika robo ya kwanza ya Mwaka 2027.

"Fedha zote za kujenga mgodi zitafadhiliwa na Perseus kupitia mikopo isiyo na riba, ambayo itapelekwa kwenye mradi wa Nyanzaga moja kwa moja. Na fedha hizo zote zipo kwani Perseus ina salio la pesa taslimu na bullion la dola za Marekani milioni 801 kufikia tarehe 31 Machi 2025" ilifafanua taarifa hiyo.

Kwa kutarajia maamuzi ya mwisho ya kuwekeza (Final Investment Decision - FID) katika mradi huo yangepitishwa na uongozi wa juu wa Kampuni ya Perseus, tayari Perseus imetumia takriban dola za Marekani milioni 27.5 katika kutekeleza shughuli za awali za maandalizi ya uwekezaji.

Shughuli hizo za awali za kujenga mradi wa Nyanzaga zilizokuwa zinaendelea ni pamoja na kama kuanzisha eneo la kufanyia kazi (site establishment), earthworks , ujenzi wa kempu pamoja na kutekeleza Mpango wa Utekelezaji wa Uhamisho (RAP) na kujenga makao mapya kwa watu walioathiriwa na mradi.

Mara baada ya kutoka kwa tangazo hilo la Perseus, Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb) amesema taarifa hiyo ni njema kwenye kukuza sekta ya madini na ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imeweka mazingira mazuri yanayoendelea kuvutia uwekezaji mkubwa nchini.

Vilevile, Mheshimiwa Mavunde alibainisha kwamba kutolewa kwa tangazo hilo na Kampuni ya Perseus kumeleta matumaini makubwa na kukata kiu ya wananchi wa Sengerema ambao wameusubiri mradi huo kwa muda mrefu na sasa ndoto yao inakwenda kutimia kwa kuona mradi mkubwa wa kuzalisha dhahabu unaanza ambao utasaidia upatikanaji wa mapato ya serikali,Ajira kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya Wilaya ya Sengerema na nchi kwa ujumla.

Aidha, Waziri Mavunde amesisitiza kwamba Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya madini nchini ili kufanikisha adhma yao na kupelekea kukuza uchumi wa Nchi na wananchi kwa ujumla.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals