[Latest Updates]: Bodi ya STAMICO Yaahidi Neema Mgodi wa Stamigold

Tarehe : Feb. 13, 2026, 10:59 a.m.
left

 Mwenyekiti akoshwa na kazi zinzaofanywa na STAMICO 

 Aahidi Serikali kuendelea kuwekeza kwenye mradi huu

Wakia 8000 za dhahanu kuzalishwa kufikia June  2026.-Ag MD

Mhe Balozi  IGP (Rtd) Simon Sirro,  Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ameendelea na ukaguzi wa miradi ya STAMICO ambapo alipata nafasi ya kufika katika Mgodi wa STAMIGOLD unaomilikiwa na STAMICO uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera. Katika ziara hiyo Mhe  Balozi Sirro amesema ameendelea kukoshwa na kazi zinazofanywa na STAMICO) huku akiahidi Serikali kuendelea  kuwekeza katika mgodi  huo.

Mhe Balozi Sirro alipata wasaa wa  kukagua maendeleo ya mgodi  na  kisha kuzungumza na Menejimenti na watumishi wa mgodi huo ambapo aliwaasa kufanya kazi kwa juhudi na   kuongeza uzalishaji ili  kuongeza  tija zaidi.

Alikiri STAMIGOLD  imepiga hatua kubwa tangu ianze Mwaka  2013 ambapo imeweza  kujitegemea kwa maana ya kuendesha shughuli zake ikiwemo manunuzi bila kutegemea fedha kutoka  Hazina.

Aidha Mhe Balozi Sirro ameiagiza STAMIGOLD kuendelea kujikita kwenye tafiti ili kubaini maeneo yanayofaa kwa uchimbaji na kuweza kupanua wigo wa uwekezaji na kufikia malengo ya kuongeza mapato.

Mhe Balozi Sirro ametumia nafasi hiyo pia kusisitiza nidhamu katika matumizi ya fedha za umma kwa watendaji walioaminiwa na kupewa nafasi mbalimbali za kusimamia na kuendesha mgodi huo.

Naye Bwn Deusdedith Magala, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO,  alisema STAMIGOLD tayari imeanza miradi mipya kwenye maeneo matatu ya uchimbaji yanayotarajiwa kuongeza uzalishaji.

Bwn Magala  alisema  ndani ya  miezi minne ijayo, hadi kufikia Juni 2026, mgodi  utazalisha wakia za dhahabu 8,000 ambazo zitaisaidia  STAMIGOLD kupiga hatua kubwa za kiuchumi.

Alisema pia STAMIGOLD imejipanga kufanya tafiti kwenye leseni ambazo hazijawahi kuguswa ili kuongeza uhai wa mgodi huo kutoka miaka mitano ijayo na kufikia zaidi ya miaka 10.

Naye  Bwn Ali Ali Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD, alisema mpaka sasa mgodi umeajiri wafanyakazi 613 ambao wanafanya kazi  na kutimiza wajibu wao  kuongeza mapato ya Mgodi.

Alisema tangu mwaka 2013, STAMIGOLD imechangia kiasi cha Tzs  Bilioni 56 serikalini na juhudi zinaendelea kuhakikisha uwekezaji uliofanyika unasaidia watanzania kupata manufaa ya mgodi.

Bwn  Ali ameihakikishia Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO kuwa utatuzi wa changamoto zilizopo utachochea kuongezeka kiwango cha uzalishaji kufikia wastani wa kilo 30 za  dhahabu kwa Mwezi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals