[Latest Updates]: Sekta ya Madini Yaweka Rekodi Mpya Makusanyo ya Maduhuli

Tarehe : June 28, 2025, 2:39 p.m.
left

Eng. SAMAMBA ASEMA HADI TAREHE YA LEO IMEKUSANYA TSH TRILIONI 1.063
Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng.Yahya Samamba amesema hadi kufikia tarehe ya leo Juni 28, 2025 Sekta ya Madini imekusanya Maduhuli ya kiasi cha shilingi Trilioni 1.063 ikiwa imebaki siku moja tu kukamilisha Mwaka wa Fedha 2024/25.

Ameyasema hayo leo Juni 28, 2025 wakati akifunga Bonanza la Wizara ya Madini lililowakutanisha pamoja watumishi wa Wizara na taasisi ambapo wameshiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, pete, riadha, kuvuta kamba,  mchezo wa kukimbia na magunia ambapo timu na watumishi walioshinda katika michezo hiyo wamepatiwa medali na vikombe.

Mwaka wa  Fedha 2024/25 Sekta ya Madini ilipangiwa kukusanya shilingi trilioni 1 ambazo zimeingizwa Mfuko Mkuu wa Serikali.

"Tumeweza kukusanya trilioni 1 na point bila kuwepo mgodi mpya. Hakuna mwaka huko nyuma tuliosogelea  shilingi 900 bilioni lakini mwaka huu tumeweza kukusanya kiasi hicho hii ikiwa ni sawa na wastani wa kukusanya shilingi bilioni 84 kila mwezi," amesema Eng. Samamba.

Ameongeza kwamba, kufuatia mwenendo mzuri wa makusanyo katika Sekta ya Madini nchini,  katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara imepangiwa kukusanya Shilingi Trilioni 1.2 na hivyo, kuwataka watumishi kuongeza bidii ili Sekta ya Madini iwe moja ya taasisi ambazo zitaongeza mapato ya ndani ya nchi yatakayoiwezesha nchi kujitegemea na kueleza, "Mhe. Rais  amesema tuongeze  makusanyo ya ndani kuiwezesha nchi kujitegemea,".

Kufuatia mafanikio hayo, Eng. Samamba amewapongeza watumishi wote wa Wizara ya Madini na taasisi zake na kueleza kuwa, mafanikio hayo yametokana na mchango wa kila mtumishi kuhakikisha kwamba malengo yaliyowekwa yanafikiwa na hivyo kuwataka kuendeleza mshikamano na kufanya kazi kwa weledi ili Sekta ya Madini iendelee kutoa manufaa ya kiuchumi kwa Taifa.

"Unapokuwa GST, TEITI, Tume  ya Madini, TGC au Wizarani  usijione siyo sehemu ya Wizara," amesema. Eng. Samamba.

Katika hatua nyingine, amepongeza hatua ya Serikali kupitia Benki  Kuu ya Tanzania ( BoT)  kuanza kununua dhahabu kama akiba ya taifa na kusema suala hilo si dogo ililinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanyika  pasipokuwepo akiba   ya dhahabu.

Pia, ameeleza kuhusu mpango wake wa kuwatembelea watumishi katika taasisi zote kwa lengo la kuzungumza nao ikiwemo kusikia changamoto walizonazo na kuahidi  kuzitafutia ufumbuzi. 

Pia, ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha watumishi kujitokeza  na kushiriki zoezi la kupiga kura wakati wa uchaguzi.

Mwisho amemtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kuweka utaratibu wa kuwa na mabonanza yasiyopungua mannne Kwa mwaka kuendelea kujenga umoja na mshikamano baina ya watumishi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo akizungumza katika bonanza hilo  amewataka watumishi kuendelea kujenga mahusiano na mawasiliano miongoni mwao huku akisititiza kujenga tabia ya kufanya mazoezi.

Naye, Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Ramadhan Lwamo amesema afya njema  inasaidia kuongeza   tija ya kazi na hivyo kuwahamasisha waendelee kufanya mazoezi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals