[Latest News]: Walivyosema Wawekezaji kuhusu Miradi ya Kimkakati

Tarehe : April 18, 2023, 4:28 p.m.
left

Kampuni tatu za uchimbaji madini kutoka nchini Australia zilisaini Hati ya Makubaliano ya Mikataba ya Uchimbaji Madini ya Kinywa na Rare Earth Elements katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma ambapo miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Morogoro, Lindi na Songwe.

Wakizungumza katika hafla hiyo Watendaji Wakuu wa  Kampuni ya Evolution Energy Ltd, EcoGraf Ltd na Peak Rare Earths Ltd walieleza kuhusu utekelezaji wa miradi yao nchini ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ameshuhudia tukio hilo Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Evolution Energy Ltd Phil Hoskins inayotarajia kuchimba madini ya Kinywe katika eneo la Chilalo wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi alisema anaamini mikataba iliyosainiwa italeta maendeleo kwa pande zote mbili.

Aidha, Hoskins amesema mkataba uliyosainiwa na Kampuni yake ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni  hiyo ambayo itachangia maendeleo katika wilaya ya Ruangwa na Taifa kwa ujumla.

Pia, Hoskins amesema Kampuni ya Evolution Energy Ltd itaendelea kufanya tafiti katika mradi wa Chilalo kwa lengo la kuongeza Maisha ya mradi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Hoskins amesema jumla ya uwekezaji wa awali katika mradi wa Chilalo ni Dola za Marekani 100 ambapo mradi unatarajiwa kuajiri zaidi ya watanzania 100 katika hatua ya ujenzi wa mradi huo.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya EcoGraf Ltd Andrew Spinks inayotarajiwa kuchimba madini ya Kinywe katika eneo la Epanko wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro alisema, katika hatua ya awali kampuni hiyo imepanga kuwekeza jumla ya Dola za Marekani Milioni 127.7 na kutoa hisa kwa serikali ya asilimia 16 zisizofifishwa na kampuni hiyo kumiliki hisa za asilimia 84. 

Pia, Mwenyekiti  wa Kampuni ya Peak Rare Earths Ltd Russel Scrimshaw inayotajia kuanza uchimbaji wa madini ya Rare Earth Element katika mradi wa Ngualla uliopo wilaya ya Songwe mkaoni Songwe alisema, Rare Earth ni madini muhimu na ni madini ya kimkakati ambayo yanatumika kutengeneza betri za magari ya umeme na matumizi mengine ya teknolojia ya kisasa.

Katika hatua nyingine, Scrimshaw alisema mradi wa Ngualla unatarajiwa kuajiri zaidi ya watanzania 300 katika kipindi cha ujenzi ambapo mradi una jumla ya uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani Milioni 437 
na inatarajia kuwa na thamani za mauzo ghafi ya kiasi cha shilingi bilioni 1,860 baada ya kuanza uzalishaji 
  
"Tunaposhuhudia mikataba ya miradi mbalimbali ya madini ikisainiwa ni kielelezo kwamba nchi imefunguka kiuchumi na kisiasa ambapo
 taifa linashuhudia wawekezaji wanamiminika nchini kitu ambacho kinaonesha uongozi na usimamizi bora wa maelekezo ya Rais Samia katika Sekta ya Madini",.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals