Tarehe : Sept. 7, 2025, 10:38 a.m.
Mwanza
Klabu ya Michezo ya Madini (MSC) imeendelea kung’ara katika mashindano ya 39 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea jijini Mwanza, baada ya kuibamiza Wakili Mkuu wa Serikali kwa ushindi wa mabao 3–1 katika mchezo wa mpira wa miguu.
Katika mchezo mwingine, timu ya wanawake ya kuvuta kamba iliiburuza Tume ya Haki kwa mvuto 1–0, na kuendeleza rekodi nzuri ya kikosi hicho.
Matokeo haya yameiwezesha Madini kutinga hatua ya 16 bora ya mashindano, hatua inayozidi kuimarisha matumaini ya klabu hiyo kufanya vizuri zaidi mwaka huu.
Mashindano yataendelea kesho, Septemba 8, 2025 ambapo Madini itapambana na Maadili katika mchezo wa mpira wa miguu, huku timu ya kamba wanawake ikitarajiwa kuvaana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita (RAS Geita).
Mbali na michezo hiyo, leo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amefungua rasmi mashindano hayo katika uwanja wa CCM Kirumba, ambapo klabu ya Madini imeungana na timu mbalimbali kushiriki katika ufunguzi huo wa heshima.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.