[Latest Updates]: Teknolojia Inayochenjua Dhahabu 98%, Mkombozi wa Uchimbaji Mdogo

Tarehe : Sept. 23, 2025, 11:30 a.m.
left

Simulizi ya Teknolojia: Dhahabu Kutoka Udongoni Hadi Sokoni

 Geita,

Katika ulimwengu wa uchimbaji mdogo, changamoto kubwa imekuwa namna ya kupata dhahabu kwa ufanisi na gharama nafuu, bila kupoteza rasilimali nyingi wala uharibifu wa mazingira na ukitumia vifaa vya kawaida na nishati kidogo kulinganisha na CIP zilizozoeleka.

Miaka kadhaa iliyopita, wachimbaji wadogo walihangaika, dhahabu nyingi ilibaki kwenye udongo, gharama za uchenjuaji zikiwa kubwa, na uharibifu wa mazingira ulionekana kutokana na njia za kijadi za kuchejulia dhahabu. 

Lakini sasa, simulizi ya ubunifu wa mtambo wa uchenjuaji madini ya dhahabu (CIP) inayotengenezwa kwa gharama nafuu ni teknolojia inayochenjua dhahabu kwa zaidi ya asilimia 98%. Mtambo huo ambao umetengezwa tofauti kidogo na ile iliyozoeleka umekuwa mkombozi wa wachimbaji wadogo.

Unapowekwa udongo wenye dhahabu ndani yake, dhahabu inatoka kwa usahihi, ufanisi, na kinachobaki ni udongo usio na madhara makubwa kwa mazingira.

John Ngeda, ni mmoja wa wabunifu wa mtambo huo, anasema kuwa, safari yake ya maarifa ilimpeleka nchini Zimbabwe, ambako alijifunza mbinu za uchenjuaji, kisha akaamua kurudi nyumbani na kuboresha teknolojia hiyo kwa manufaa ya wachimbaji wa Tanzania. 

Matokeo yake yamekuwa makubwa kwani zaidi ya mitambo 25 imejengwa katika Kanda ya Ziwa pekee, na sasa ipo hadi Mbeya na Mpanda.

Wachimbaji wadogo wanaona utofauti si tu kwamba wanapata dhahabu zaidi, bali pia wanaokoa gharama kubwa walizokuwa wakitumia kwa njia zisizo na tija. Mazingira pia yanapumua, kwa sababu teknolojia hii ni rafiki wa mazingira, ikipunguza madhara yaliyokuwa yakisababishwa na kemikali hatarishi.

Katika Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Geita tarehe 23 Septemba 2025, mtambo wa CIP umegeuka kivutio kikuu. Wananchi wanapata kushuhudia jinsi teknolojia hiyo ilivyobadilisha maisha ya wachimbaji wadogo kutoka hali ya kuchimba kwa mazoea na hatimaye kuchimba kwa tija zaidi.

Hii siyo tu simulizi ya dhahabu, bali ni simulizi ya ubunifu wa Mtanzania, na ushindi wa teknolojia rafiki kwa binadamu na mazingira.

Dhahabu sio ndoto au madini yanayoambatana na ushirikina bali ni urithi unaleta maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi pia huku ikibadili maisha ya maelfu.

Dhahabu haipo tu ardhini; ipo pia kwenye mawazo ya wabunifu wanaothubutu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals