[Latest Updates]: Tanzania Itaendelea Kuweka Kipaumbele Kwenye Madini Mkakati - Mbibo

Tarehe : June 25, 2025, 2:14 p.m.
left

Dar es Salaam

Tanzania imeweka mkakati thabiti wa kuipa kipaumbele Sekta ya Madini , hasa madini yenye thamani ya kimkakati kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kuongeza ajira na kuongeza thamani ya Pato la Taifa.

Hayo yalisemwa Juni 24, 2025 na Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo wakati akifungua mkutano wa Jiolojia Barani Afrika (PanAfGeo).

Mbibo alieleza kuwa, Tanzania imepanga kuendeleza utafiti wa Jiosayansi ambapo imepanga ifikapo mwaka 2030 kufikia asilimia 50 kwa utafiti wa jiofizikia.

Akielezea kuhusu uongezaji thamani madini , Mbibo alieleza kuwa, mkakati mwingine ni kujenga viwanda vya kuchakata madini ya kimkakati yakiwemo madini ya Kinywe, nikeli, lithium pamoja na madini ya shaba.

Kuhusu ushirikiano wa kimataifa kwenye Sekta ya Madini, Mbibo alifafanua kuwa,Tanzania inaendelea kuongeza ushirikiano na taasisi mbalimbali za kimatsaifa  ikiwemo Umoja wa Ulaya hususani kwenye Sekta ya Madini kwa lengo la kuongeza na ujuzi kwa watalaam wa jiolojia nchini.

Mbibo aliongeza kuwa, kuwepo kwa  ushirikiano wa kimataifa kwa EU na nchi nyingine unaongeza nguvu kubwa katika nyanja mbalimbali ndani ya mnyororo mzima wa utafiti wa Jiosayansi na kuibua sehemu mpya za uwekezaji nchini na Afrika kwa ujumla.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals