Tarehe : Feb. 5, 2026, 2:53 p.m.
Wanafunzi Mpwapwa Sekondari wajifunza na kujionea aina za Miamba ya Madini.
Dodoma.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mpwampwa wametembelea Makumbusho ya Jiolojia Pamoja na Maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania- GST kwa lengo la kujifunza na kujionea Miamba na Madini mbalimbali inayopatikana nchini. Aidha, wanafunzi hao wamepata fursa ya kutembelea Maabara ya Taasisi hiyo na kujifunza namna inavyofanya kazi ya uchunguzi wa Sampuli mbalimbali za Madini.
Wakizungumza Leo Februari 5, 2026 Jijini Dodoma kwa niaba ya wenzao baada ya kutembelea Makumbusho hayo ya GST Bruno Hendry na Denis Dickson wameipongeza GST kwa kuwa na makumbusho mazuri yenye kuonesha miamba ya Madini mbalimbali yanayopatikana hapa nchini.
Aidha, wanafunzi hao wamesema wamepata fursa ya kuona ramani inayoonesha Mikoa yenye madini na aina za madini yanayopatika katika mikoa hiyo.
Pia, Wanafunzi hao walipata fursa ya kutembelea maabara ya GST na kujionea vifaa vya kisasa na namna uchunguzi wa madini katika sampuli mbalimbali unavyofanyika katika maabara hiyo.
Naye Mwalimu Justine Damas ameishukuru GST kwa kuwapa fursa wanafunzi wetu kuweza kujifunza kwa vitendo kwa kuona aina za miamba mbalimbali ya Madini yanayopatikana hapa Nchini.
"Niwashukuru sana GST kwa fursa hii, nimefurahi sana kwa kwa sababu wanafunzi wangu leo wameona na kujifunza miamba mbalimbali inayopatikana nchini kwani mara nyingi tunafundisha kwa nadharia" Alisema Mwl. Damas.
Naye mtaalam wa GST ambaye alikuwa anatoa mafunzo kwa wanafunzi hao Bw. Andrew Buluba ambaye ni mjiolojia amewashukuru wanafunzi hao kwa kuitembelea GST na kuwakaribisha tena watakapo hitaji elimu hiyo.
Makumbusho ya Jiolojia ya GST ni makumbusho yaliyosheheni sampuli za miamba na madini yanayopatikana nchini.
Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya kati na vya juu pamoja na wadau wengine mara nyingi wamekuwa wakitembelea makumbusho hayo ili kujionea na kujifunza miamba na madini yanayopatikana nchini.
Mwisho
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.