[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yaja na Programu ya Mining for Brighter Tomorrow (MBT) kwa Ajili ya Wachimbaji Vijana na Wanawake

Tarehe : April 8, 2024, 10:14 p.m.
left

-Itahusisha utoaji wa Leseni ya maeneo ya uchimbaji_

-Wachimbaji kunufaika na Magari,Vifaa  na Mitambo_

-Aitaka Menejimenti ya Wizara ya Madini kusimamia utekelezaji wa miradi ya wachimbaji

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema Serikali itatekeleza programu ya Mining for a Brighter (MBT) kwa lengo la kuwainua wachimbaji wanawake na vijana.

Mhe. Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 08 Aprili, 2024 Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyanyakazi wa Wizara na Taasisi zake na kutumia fursa hiyo  kuwataka viongozi na watumishi wa Wizara kuwa wabunifu kila wakati wanapotekeleza majukumu yao.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuiimarisha wizara ya madini kwa kuitengea fedha za kutekeleza miradi na mipango mbalimbali," amesema Mavunde.

Amesema Mpango mahsusi ambao Wizara inakuja nao sasa ni kuwaendeleza wachimbaji wakinamama na Vijana Kupitia programu ya Mining for A Brighter Tomorrow(MBT) yenye lengo la kuwapatia leseni za maeneo ya uchimbaji, magari, vifaa na mitambo ya uchimbaji.

Amesema kupitia programu hiyo itasaidia kuchochea ukuaji wa sekta ya madini, uchumi wa Taifa na kuongeza ajira kwa watanzania.

"Tumieni hili Baraza la wafanyakazi kuhakikisha mnakuja na mpango mzuri wa kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi chini ya Wizara," Amesisitiza Mavunde.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwapongeza  Watumishi Wa Wizara kwa jitihada za ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kueleza kuwa ana imani kubwa kwa watumishi wa Wizara kuwezesha Sekta ya Madini kufikia mchango wa asilimia 10 kwenye pato la Taifa ifikapo 2025.

Awali, akimkaribisha Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Waziri wa Madini amewapongeza watumishi wote wa Wizara kwa namna wanavyoendelea kujitolea kuhakikisha mikakati yote ya kuendeleza Sekta ya Madini inafanikiwa.

Naye,  Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo ameeleza kwamba Baraza hilo ni utekelezaji wa wajibu wa mwajiri kwa wafanyakazi na kubainisha kuwa mkutano huo umelenga zaidi katika kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na mpango wa bajeti ijayo ya mwaka 2024/2025.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals