[Latest Updates]: Dhahabu Kilo 9 Iliyokuwa Inatoroshwa Yakamatwa Jijini Mbeya

Tarehe : March 19, 2024, 12:23 p.m.
left

Waziri Mavunde aingia mtaani na kikosi kazi kwenye eneo la maficho

Aupongeza Uongozi wa Mkoa na Vyombo vya Usalama Mbeya

Aagiza kusimamisha Leseni za biashara ya Madini za watuhumiwa

Dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya Tsh 1,555,476,586

Serikali ingepata mapato ya Tsh 144,659,322

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia wafanyabiashara wa madini 10 kwa tuhuma za utoroshaji wa madini Kilogramu 9.8 yenye thamani ya Tsh 1,555,476,586.

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari,Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema wafanyabiashara hao walikamatwa siku ya Jumamosi saa 10:27 Alfajiri Katika mtaa wa Ilomba Jijini Mbeya  kwenye nyumba waliyokuwa wamepanga wakiwa na vipande 344 ya dhahabu iliyochomwa yenye uzito wa Kilogramu 9.8 pamoja  na vifaa mbalimbali kama vile Precious Metal analayzer (XRF) aina ya Niton DXL thermoscientific, mitungi ya gesi, jiko na vyungu kwa ajili ya kuchomea dhahabu, Kipimo cha maji cha kupimia dhahabu, mizani kadhaa pamoja na kemikali aina ya borax.

Mhe. Mavunde ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Mbeya chini ya Mh. Juma Homera na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kufanikisha ukamataji wa watuhumiwa hao.

Pia, Waziri Mavunde ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wa madini kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za kufanya biashara ya madini nchini na wote watakaobainika kutorosha madini watachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kufutiwa Leseni zao.

Aidha, Waziri Mavunde ameagiza kusimamishwa kwa Leseni za biashara ya Madini za watuhumiwa nchi nzima wakati taratibu za upepelezi zikiendelea kabla ya kufikishwa Mahakamani.

Akizungumza katika zoezi hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya wa Chunya Mhe. Mbaraka Batenga amewataka viongozi wote wa mitaa na vijiji kuwatambua watu katika maeneo yao kwa kuwasajili katika daftari la wakazi na kuwataka wamiliki wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanawafahamu vyema wapangishaji wao na shughuli zao.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals