[Latest Updates]: Sekta ya Madini Kitovu cha Uchumi Nchini

Tarehe : June 13, 2025, 5:40 p.m.
left

Ruangwa, Lindi

Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amesema kuwa, maendeleo ya Sekta ya Madini yanapelekea kuwa kitovu cha uchumi nchini, hii ni kutokana na mageuzi mbalimbali yanayoendelea kufanyika.

Dkt.Kiruswa ameyasema hayo leo Juni 13, 2025, wakati akizungumza na vyombo vya habari mapema baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya madini yanayoendelea kufanyika  wilayani Ruangwa.  

Akielezea kuhusu uwekezaji wa ndani Dkt.Kiruswa ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa kivutio kikubwa  cha wawekezaji katika Sekta ya Madini kutokana na utajiri wake wa madini mbalimbali yakiwemo madini ya kinywe,makaa ya mawe pamoja na madini adimu na madini mkakati.

Kuhusu kukua kwa Sekta ya Madini, Dkt. Kiruswa amebainisha kuwa, Sekta hii imeendelea kukua kwa kasi  ambapo kwa sasa inachangia asilimia 10.1 kwenye Pato la Taifa.

Dkt.Kiruswa ameongeza kuwa, ukuaji huu unatokana mipango endelevu hususan katika  uongezaji thamani madini, uwekezaji wa mitaji ya ndani na nje ya nje pamoja na Sera madhubuti za  usimamizi wa rasilimali madini nchini.

Pamoja na mambo mengine, Serikali imeendelea kusisitiza  kuhusu uongezaji thamani madini kufanyika ndanibya nchi kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, ujenzi wa viwanda vya kusafisha dhahabu, ujenzi wa maabara za uchenjuaji na uchakataji madini.

# MineralValueAddition
#GDP:10.1%FromMineralSector
#Vision2030:MadiniNiMaishaNaUtajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals