[Latest Updates]: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC Yaipongeza STAMICO

Tarehe : Feb. 21, 2024, 11:59 a.m.
left

Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imetembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichopo jijini Mwanza  leo tarehe 20  Februali,2024 na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi 

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake  Ndugu Deus Clement Sangu imeona  maendeleo mazuri ya usafishaji wa dhahabu kiwandani hapo ikilinganishwa na kipindi  cha nyuma walipotembelea kiwandani hapo

 Aidha Mwenyekiti wa Kamati ameipongeza Serikali  kupitia STAMICO  kwa  kuongeza mapato yake pamoja na kuanzisha kiwanda hicho ambacho kitapelekea  STAMICO kupata mapato na nchi kupata  faida mbalimbali kutokana  na usafishaji wa  dhahabu nchini
 

Katika wasilisho lake la kamati Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO   Dkt Venance Mwasse alielezea utekelezaji  wa shughuli za kiwanda pamoja na changamoto  ya kiwanda  ya  kutokupata dhahabu ghafi   kwa wingi kutokana  na maswala mbalimbali ikiwemo changamoto ya kikodi.

Kamati iliahidib kuifanyia kazi changamoto hii ya kikodi kwa kushirikiana na Serikali  ili kiwanda kiweze  kupata malighafi ya kutosha na kufanya kazi vizuri

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO  Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo aliishukuru kamati ya PIC kwa ushauri wao wanaoutoa mara kwa mara kwa  Shirika kuhusu maswala ya uwekezaji  nakupelekea  Shirika kuendelea kufanya  vizuri

Ziara   hii ya Kamati itahusisha kutembelea miradi mingine ya Shirika ya STAMIGOLD na  Makaa ya mawe Kiwira ili  wajumbe wajionee uwekezaji wa STAMICO  katika miradi mbalimbali.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals