[Latest Updates]: Wadau Waitikia Wito wa Uongezaji Thamani Madini

Tarehe : April 3, 2025, 12:38 p.m.
left

Ni utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan

Kiwanda cha kuchakata madini ya shaba chajengwa Wilayani Chunya,

Serikali yaahidi kuwezesha viwanda zaidi vya uongezaji thamani madini

Wachimbaji wadogo kunufaika na soko la uhakika la Madini Shaba

Kufuatia utekelezaji wa Mkakati wa kutosafirisha madini ghafi nje ya Nchi, Serikali yapongeza Wadau kwa kuitikia wito wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia S. Hassan wa kujenga viwanda vya uongezaji thamani madini nchini.

Hayo yemesemwa leo na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde (Mb) alipotembelea kujionea ujenzi wa kiwanda cha uongezaji thamani madini ya shaba kilichopo Kata ya Mbugani Wilayani Chunya kinachomilikiwa na Kampuni ya Mineral Access System Tanzania (MAST).

"Mh. Rais ametuelekezaee kuhakikishia tunasimamia Sheria na Kanuni ili kuwezesha madini kuongezwa thamani hapa nchini kabla yayajasafirishwa nje ili nchi kunufaika na sekta ya madini.

"Tutaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa wadau na wawekezaji wengine walio tayari kuunga mkono jitihada hizi za Mhe. Rais ili kama Nchi tupate manufaa zaidi ya kiuchumi ikiwemo kuongeza upatikanaji wa ajira kwa wananchi wetu na kukuza pato la Taifa" alibainisha Mhe. Mavunde.

Aidha, Waziri Mavunde alieleza kuwa madini ya shaba yanahitaji kuongezwa kiwango kwa kuchakatwa kufikia asilimia 20 au zaidi ili yaweze kuuzwa nje, Ile hali madini yanayopatikana nchini yana kati ya 0.5% mpaka 2%, na kwamba kiwanda kitakuwa kinazalisha shaba kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 70, ambapo alisisitiza ni mageuzi makubwa sana ya kiuchumi nchini.

Vilevile, Waziri Mavunde alioneshwa kufurahishwa na mpango wa Kiwanda cha MAST wa kuhudumia wachimbaji wadogo kupitia kutoa elimu, kugharamia uchimbaji na kuwa soko la shaba yao ya kiwango cha chini ambayo awali walikuwa wakihangaika na soko. Hili litakuwa ni suluhisho tosha kwa wachimbaji wadogo kwani nguvu zao hazitakwenda bure.

Akisisitiza mikakati ya Serikali kwa wachimbaji wadogo, Mhe. Mavunde alibainisha kuwa Wizara ipo mbioni kuanzisha Vituo vya ukodishaji wa mitambo ya uchimbaji Nchi nzima ili kusogeza huduma hiyo kwa wachimbaji wadogo na kwa gharama nafuu.

Awali, akimkaribisha Waziri katika kiwanda hicho, Bw. Georgefrey Kente, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MAST aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kuahidi kwamba Kampuni yake inakwenda kujenga viwanda vingine kama hivyo katika Mkoa wa Dodoma na Lindi ili kufikia malengo yao ya uzalishaji.

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Chunya ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya, Bw. Michombero Anakleth aliishukuru Serikali kwa kuwezesha ujenzi wa kiwanda hicho kwa kasi kubwa na kueleza bayana kuwa Uongozi wa Wilaya ya Chunya unaunga mkono kwa asilimia 100 zoezi la ufutaji wa leseni za madini zisizoendelezwa ili wapewe wawekezaji wenye nia njema kwa manufaa ya Nchi yetu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals