[Latest Updates]: Watumishi Wanawake TEITI Waadhimisha Siku Yao Duniani

Tarehe : March 8, 2024, 1:22 p.m.
left

Waziri Gwajima atoa wito kwa Wanawake. 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa Wanawake kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuwa wanauwezo wa kufanya kazi nyingi  kwa umakini na kwa uaminifu mkubwa.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Machi 8, 2024 katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kilichofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali II iliyopo Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

"Mwanamke ni Mama pia ni Kiongozi na ni mshauri mzuri katika jamii hivyo ni wasihi wanawake wenzangu tuendelea kuchapa kazi bila woga na tusichague  kazi pia tusijihisi kwamba hatuwezi kufanya kazi fulani," amesema Dkt. Gwajima.

Kwa Upande wake Jacqueline Aloyce ambaye ni Kaimu Huduma wa Taasisi ya Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) amewataka wanawake wa Taasisi hiyo kuendelea kujitokeza kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuongeza mchango wa wanawake kwenye maendeleo ya Taifa na kusimamia Sheria ya TEITA Act ya mwaka 2015 na vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji EITI na kuhakikisha Miongozi na Taratibu  zote za Serikali zinafuatwa.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yanafanyika jijini Dodoma ambayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo "Wekeza Kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa na Ustawi wa Jamii".

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals