[Latest Updates]: Wabunge wa Zambia Wavutiwa na Mfumo wa Masoko ya Madini Tanzania

Tarehe : April 10, 2025, 7:26 p.m.
left

Dodoma

Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Uchumi wa Taifa, Biashara na Kazi kutoka Bunge la Taifa la Zambia umewasili nchini Tanzania kwa ziara ya mafunzo ya kikazi, yenye lengo la kujifunza mbinu na mifumo bora ya usimamizi na uendeshaji wa Sekta ya Madini, sekta ambayo imeendelea kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania katika miaka ya hivi karibu.

Tanzania imekuwa kivutio kwa mataifa mbalimbali kusini mwa Jangwa la Sahara, kutokana na mageuzi makubwa yanayofanywa katika sekta hiyo chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mageuzi hayo yamelenga kuimarisha utawala bora wa rasilimali madini, kuwajengea uwezo wachimbaji wa ndani, na kuvutia wawekezaji wa kimataifa kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji.

Baada ya kuwasili nchini na Kupokelewa na Waziri wa Madini Mhe.  Anthony Mavunde Aprili 9, 2025, Ujumbe huo leo Aprili 10 2025 ulipata nafasi ya kusikiliza wasilisho kutoka Tume ya Madini kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini hapa nchini pamoja na vituo vya ununuzi wa madini.

Awali akizungumza Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ushirikishwaji wa Watanzania (local content) pamoja Wajibu wa Kampuni kwa Jamii inayozunguka miradi (CSR) Terence Ngole ameeleza kamati hiyo kuwa Tanzania imeanzisha masoko ya madini 43 na vituo vya ununuzi zaidi ya 109 nchi nzima na kwamba uanzishwaji wa masoko hayo umechangia kuondoa tatizo la utoroshaji wa madini, kuongeza mapato ya Serikali kupitia kodi, na kuwapa wachimbaji uhakika wa bei nzuri na soko la uhakika kwa madini yao.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe wa Bunge la Zambia, Mhe. Bi. Sibeso Kakoma Sefulo, amesema kuwa Zambia ilichagua kuja kujifunza kutoka Tanzania kutokana na mafanikio makubwa ambayo Tanzania imeyapata katika uboreshaji wa sekta ya madini.

Amesema kuwa mfumo wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini umewavutia sana na ni moja kati ya vitu watakavyochukua na kwenda kuishauri Serikali ya Zambia kwa kuwa kimeleta manufaa makubwa Tanzania.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals