[Latest Updates]: STAMICO Yajipanga Kuwa Shirika Lenya Mauzo ya Shilingi Trilioni

Tarehe : June 25, 2025, 2:09 p.m.
left

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO), limesema kwa sasa sio tegemezi tena na lina mipango ya kwenda mbele zaidi ikiwa ni pamoja na kufanya uwekezaji mkubwa kimataifa.

Kauli hiyo ilitolewa Juni 24, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, wakati wa kuzindua mitambo 10 ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini vyenye thamani ya Sh bilioni 12.41 kwa ajili ya  shirika hilo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema kupitia mkakati huo uliowekwa, ifikapo mwaka 2030 litakuwa Shirika la madini la Daraja la Viwango vya Dunia (World Class State Mining Corporation) na kwamba litakuwa ni shirika lenye mauzo ya trilioni nyingi za fedha.

“Shirika la Madini tumeshaondoka kwenye utegemezi, tumeshaachana na kuwa kwenye Comfort Zone, tunaanza safari ya kuwa World Class State Mining Corporation ambayo kupitia andiko letu na slogan yetu ya MASTASHA (Make STAMICO Shine Again) tunakwenda kuwa Multi Trillion Turnover Corporation (Shirika la mauzo ya Trilioni nyingi) ifikapo 2030,” amesema  Dr  Venance Mwasse.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals