[Latest Updates]: Kiwanda cha kusafisha dhahabu Chunya mbioni, Serikali yatimiza ahadi

Tarehe : Oct. 9, 2025, 4:36 p.m.
left

Chunya, Mkoa wa Pili wa Kimadini kwa uzalishaji wa dhahabu nchini baada ya Geita, imepiga hatua kubwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu cha Giant Equipment and Machine’s Limited. Kiwanda hiki kina uwezo wa kusafisha kilo 20 za dhahabu kwa siku kwa usafi (purity) wa asilimia 99.9 na kiko mbioni kuanza uzalishaji rasmi, baada ya kukamilika kwa baadhi ya taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) .

Akizungumza katika mahojiano maalum na timu ya Madini Diary kutoka Wizara ya Madini Oktoba 8, 2025,  Meneja Uendeshaji wa Kampuni hiyo Hassan Pazi amesema tayari majaribio ya kusafisha dhahabu kiwandani hapo yamefanyika kwa awamu tatu tofauti na zote zimetoa matokeo ya kiwango cha kusafisha hadi asilimia 99.9, jambo linaloashiria kuwa dhahabu inayosafishwa na kiwanda hicho inakidhi vigezo vya kununuliwa na BoT kutumika kama amana ya Serikali  na kusafirishwa nje.

‘’Awamu zote zilionesha purity ya asilimia 99.9 hii ni kiashiria tosha kwamba mashine zetu ziko vizuri na tumefikia lengo letu hivyo, wachimbaji wawe tayari muda si mrefu tutaanza rasmi kusafisha dhahabu hapa Chunya. Kwa sasa zipo taratibu tunazikamilisha na BoT,’’ amesema Pazi.

Ameongeza kwamba, hatua ya Chunya kuanza kusafisha dhahabu itasaidia kupunguza adha ya wachimbaji na wafanyabiashara kusafiri umbali mrefu hadi katika mikoa ya Dodoma, Geita na Mwanza kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Kutokana na hatua iliyofikiwa na kampuni hiyo, imeipongeza Serikali kwa kutoa eneo ambalo limewezesha kujengwa kwa kiwanda hicho  ikiwemo kutembelewa mara kwa mara na wataalam kwa ajili ya ushauri na maelekezo yaliyowezsha kukamilisha taratibu zote.

Akizungumzia kuhusu  ajira, Pazi amesema kiwanda hicho kitaendeshwa kwa asilimia 100 na watanzania na kwamba watalamu wa kitanzania walihusika katika hatua zote tangu ujenzi  kikihusisha wahandisi, watoa huduma na wajenzi hadi kufikia hatua ya kuelekea kwenye uzalishaji.


 Mbali na kusafisha dhahabu, kampuni hiyo inamiliki kiwanda cha kuchenjua dhahabu chenye mitambo ya uwezo wa kubeba kilo 650 za kaboni kila mmoja. Pia, kampuni hiyo inajihusisha na biashara ya kuuza kemikali za aina zote, vifaa kinga na kudhamini wachimbaji wadogo.

Kukamilika kwa kiwanda hicho kunaendelea kuonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya kuongeza thamani ya madini hapa nchini na kutekeleza mikakati ya sekta hiyo kwa vitendo. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alikielezea kiwanda hicho bungeni katika hotuba ya bajeti ya mwaka 2025/26 na sasa, ahadi hizo zimetia mwanzoni tu mwa robo ya pili ya mwaka.

Mbali na kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Chunya, Serikali itanufaika kupitia kodi na tozo mbalimbali  sambamba na Halmashauri ya Wilaya ambayo itanufaika moja kwa moja na mapato yatokanayo na shughuli za kiwanda.

Kukamilika kwa kiwanda hichi kunafanya idadi ya viwanda vya kusafisha dhahabu nchini kufikia vinane.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Features Images
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals