[Latest Updates]: Wachimbaji Wadogo Mbogwe Washauriwa Kufuata Kanuni za Msaada wa Kiufundi

Tarehe : March 14, 2026, 12:49 p.m.
left

Mbogwe , Geita

Wachimbaji wadogo wa madini  Mkoa wa kimadini Mbogwe wametakiwa kuzingatia Kanuni za Msaada wa Kiufundi  zilizotangazwa na Serikali ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuepuka migogoro isiyo ya lazima na wawekezaji.

Rai hiyo ilitolewa Machi 13, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa  wakati wa ziara yake ya kikazi katika mgodi wa Peter Kisura Kawe na Washirika uliopo wilayani Mbogwe.

Dkt. Kiruswa alisema kuwa ni vyema kuzingatia Kanuni mpya za mwaka 2025 zinazoratibu ushiriki wa watoa msaada wa kiufundi katika leseni ndogo za uchimbaji.

Dkt.Kiruswa alieleza kuwa , mikataba yote ya msaada wa kiufundi kati ya mchimbaji mdogo na mtoa huduma lazima isajiliwe rasmi Tume ya Madini.

Dkt.Kiruswa alifafanua kuwa kanuni zinaelekeza kuwepo kwa uwazi katika mgawanyo wa mapato ya madini yatakayozalishwa ili kumlinda mchimbaji mdogo.

Aliongeza kuwa , msaada wa kiufundi  unapaswa kulenga kuongeza ujuzi, kutoa teknolojia ya kisasa, na kuongeza kiasi cha madini kinachopatikana.

Dkt.Kiruswa alisisitiza kuwa,wachimbaji wadogo 
wana fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu kupitia programu maalum za kibenki kama CRDB Bank zilizozinduliwa hivi karibuni.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa kimadini Mbogwe Mhandisi Ludovick Mwacha alisema mpaka sasa mkoa wa kimadini Mbogwe umefikia asilimia 75.81 makusanyo ya lengo la Mwaka 2025/2026.

Awali, akitoa taarifa ya mwenendo wa uzalishaji katika mgodi wa Peter kisura na Washirika , Meneja Mgodi  Mhandisi  Samson Mathias  alisema, mgodi ulianza  uzalishaji rasmi  mwaka 2025 na mpaka sasa unazalisha kilogram 8 kwa mwezi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals