[Latest Updates]: Mgodi wa ZEM wapewa siku saba kutoa vifaa vya kujikinga

Tarehe : March 28, 2018, 10:39 a.m.
left

Serikali imetoa siku Saba kwa Mgodi wa Dhahabu wa ZEM (T) Company Ltd wa Nyasirori Wilayani Butiama kuwapatia vifaa vya kujikinga kazini (safety gears) wafanyakazi wa mgodi huo vinginevyo mgodi utafungwa.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akitembelea Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited alipofanya ziara mgodini hapo kujionea shughuli ziazoendelea. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi.[/caption]

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye mgodi huo kujionea shughuli zinazoendelea mgodini hapo na kuzungumza na wafanyakazi na wananchi wanaozunguka maeneo jirani na mgodi huo.

Wafanyakazi na wananchi wanaozunguka mgodi huo walimueleza Naibu Waziri huyo changamoto mbalimbali walizonazo kutokana na shughuli za mgodi ikiwemo mahusiano mabaya na wananchi, wafanyakazi kukosa vifaa vya kujikinga, mishahara midogo na manyanyaso ikiwemo kupigwa.

Akitoa tamko kuhusiana na hoja hizo zilizowasilishwa kwake, Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kufanya shughuli zake kwa kufuata utaratibu, kanuni na sheria za Nchi.

Alisema haiwezekani wafanyakazi wakafanya shughuli mgodini hapo bila kuwa na vifaa vya kujikinga na aliiagiza Ofisi ya Madini Musoma kufuatilia suala hilo na endapo siku hizo zitapita bila vifaa hivyo kuletwa afunge mgodi.

“Ninawapa Siku Saba wawe wameleta vifaa na wasipofanya hivyo funga mgodi, ni lazima wafanyakazi wapatiwe vifaa vya kujikinga, kulingana na kazi wanazofanya,” alisema Nyongo.

Akizungumzia suala la mishahara, Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kuhakikisha unafuata Sheria ya Madini inavyoelekeza kwa kuwalipa mshahara stahiki ambao alisema kima cha chini kuwa ni 400,000.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited uliopo Butiama, Mkoani Mara (hawapo pichani) wakati wa ziara yake mgodini hapo. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina.[/caption]

Naibu Waziri Nyongo vilevile aliuagiza mgodi huo kuandaa mikataba ya ajira na kwamba atakapofanya tena ziara mgodini hapo akute wafanyakazi wanayo mikataba ya ajira iliyoandaliwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha, aliuonya mgodi huo tabia ya kupiga wafanyakazi, alisema jambo hilo halikubaliki na ni kinyume na utu wa binaadamu na kwamba ikitokea mfanyakazi akapigwa, Ofisi ya Madini ifunge mgodi huo mara moja.

“Ni marufuku kupiga wafanyakazi, atakayepigwa aende Polisi na sisi tutaufunga mgodi. Mkuu wa Wilaya yupo hapa muwe mnamueleza matatizo yenu ili yapatiwe ufumbuzi,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Butiama kusimamia vyema masuala yote ya ulinzi na usalama, na ahakikishe anatembelea mgodini hapo ili kuzungumza na wafanyakazi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Vilevile Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kutofukuza mfanyakazi yoyote aliyeeleza changamoto zinazowakabili kwenye utekelezaji wa majukumu yao. “Usimfukuze mfanyakazi yoyote aliyetoa kero yake katika ziara hii, wako huru kuzungumza nami,” alionya Naibu Waziri Nyongo.

Kuhusu suala la mahusiano na wananchi, Nyongo aliuagiza mgodi huo kuajiri mtu maalum wa mahusiano atakayefanya mawasiliano ya mara kwa mara na wananchi ili kuboresha mahusiano na hapohapo aliiagiza Serikali ya Kijiji kufanya mikutano ya mara kwa mara na wanachi ili kuwapatia mrejesho wa masuala mbalimbali baina ya mgodi na maendeleo ya kijiji.

Imeandaliwa na:

Mohamed Saif,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals