[Latest Updates]: Naibu Waziri Biteko akutana na wachimbaji madini Lugoba

Tarehe : May 7, 2018, 10:11 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 06 Mei, 2018 amekutana na wachimbaji wa madini ya ujenzi aina ya kokoto katika eneo la Lugoba wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Mkutano huo uliohusisha Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na wananchi, ulilenga kujadili changamoto katika uchimbaji madini ya ujenzi aina ya kokoto.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM) akielezea shughuli za uchimbaji wa madini ya kokoto kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika eneo la Lugoba wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.[/caption]

Katika mkutano huo, Naibu Waziri Biteko alitoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na wawekezaji  kuendeleza maeneo yao,  wawekezaji kutouza leseni kwa mtu mwingine pasipo kushirikisha serikali,    wawekezaji kuandaa mpango wa utoaji huduma kwa jamii pamoja na kuutekeleza na  Ofisi ya Madini ya Kanda ya Mashariki kufuatilia ahadi za wawekezaji katika huduma za jamii na kuwasilisha  ripoti mara moja.

Maelekezo mengine ni pamoja na Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki kuwasilisha  ripoti ya athari za mazingira kabla ya Mei 20, 2018, wawekezaji kushirikiana na wananchi wanaowazunguka, kampuni zenye mgogoro na wananchi kuhakikisha zinamaliza tofauti zao na fedha za halmashauri  kutumika kwenye uwekezaji mwingine kwa ajili ya maendeleo.

Imeandaliwa na:

Greyson Mwase,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals