[Latest Updates]: Serikali Imebaini Maeneo Manne ya Changamoto kwa Wachimbaji- Dkt. Kiruswa

Tarehe : May 11, 2024, 5:03 p.m.
left

SERIKALI IMEBAINI MAENEO  MANNE YA CHANGAMOTO KWA WACHIMBAJI- DKT. KIRUSWA

Dodoma

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema kufuatia utafiti uliofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika mikoa tisa (9) nchini, Serikali imeweza kubaini maeneo manne ya changamoto zinazowakibili wachimbaji wadogo wa madini wakiwemo wa Singida Mashariki.

Dkt. Kiruswa ameyasema hayo leo Mei 10, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Nusrat Hanje kwa niaba ya Waziri wa Madini Anthony Mavunde, katika swali lake la msingi, Mhe. Nusrat Hanje alitaka kujua ni lini Serikali itawezesha Wachimbaji Wadogo wa Madini Singida Mashariki.

‘’Mheshimiwa Spika, changamoto hizo ni pamoja na kutokuwa na uelewa kuhusu Sheria na Kanuni za sekta ya madini, taarifa za kijiolojia ya maeneo wanayochimba, mitaji na upatikanaji wa maeneo ya kuchimba madini,’’ amesema Dkt. Kiruswa.

Ameongeza kwamba, Serikali imeendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo kutatua changamoto hizo kwa kutoa elimu, kuwapatia vifaa vya uchorongaji, kuwaunganisha na taasisi za kutoa mikopo na vifaa vya uchimbaji sambamba na kutenga maeneo mahsusi kwa ajili yao, na kueleza, ‘’ wachimbaji wadogo wa Singida Mashariki wako katika mpango endelevu wa Serikali wa kuwezeshwa ili waweze kufanya uchimbaji wenye tija,”.

Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, mpango huo endelevu wa kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa manufaa zaidi pia unajumuisha wachimbaji wadogo kutoka maeneo mbalimbali tofauti hapa nchini.

Akizungumzia malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha Mradi wa Singida Gold Mine unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold Mining, Dkt. Kiruswa amesema kuwa tayari mgodi huo umekwishawalipa wananchi waliokuwa wakiishi eneo la mgodi, lakini kwa wale baadhi waliopo katika eneo la leseni mchakato wa kuwalipa fidia unaendelea mwaka huu.

#Kutoka BungeniDodoma

#Vision2030: MadininiMaishanaUtajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals