Tarehe : June 4, 2024, 12:19 p.m.
-Menejimenti ya Wizara yamtaka mkandarasi wa mradi kuongeza kasi
Ujenzi wa Jengo la ofisi ya Wizara ya Madini katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma umefikia asilimia 82 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2024.
Hilo limebainishwa leo Juni 4, 2024 na Meneja wa mradi huo, Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambaye ni Mkandarasi wakati akielezea maendeleo ya mradi mbele ya Menejimenti ya Wizara ya Madini iliyomtembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Madini, Festus Mbwilo amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa wakati.
Aidha, Mbwilo amemtaka mkandarasi kutosita kuwasiliana na Wizara pale wanapokumbana na changamoto yeyote ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.