[Latest Updates]: Tunapata Ushirikiano Mkubwa Kutoka Serikalini, Wananchi -WDL

Tarehe : Feb. 7, 2024, 8:02 a.m.
left

 

DKT. KIRUSWA AMWAKIKISHIA UTATUZI WA CHANGAMOTO

CapeTown

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds na Mwenyekiti wa Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, inayofanya shughuli za Uchimbaji wa Madini ya Almasi Mwadui Richard Duffy, ameishukuru Serikali ya Tanzania kufuatia ushirikiano ambao inaendelea kuupata kwenye uwekezaji wa kampuni hiyo nchini.

Ameongeza kuwa,  katika kipindi cha miaka mitano, kampuni hiyo imeshuhudia mabadiliko makubwa yenye tija yakihusisha mahusiano mazuri ambayo kampuni hiyo inayapata kutoka kwenye jamii inayozunguka mgodi huo.

Amesema Mgodi huo utaendelea kufanya shughuli zake kwa kushirikiana na jamii inayouzunguka na kuongeza kwamba, ni moja ya migodi ya kiwango cha juu duniani.

Aidha, Duffy amemweleza Naibu Waziri kuhusu changamoto ambazo mgodi huo inakabiliana nazo na kuiomba   Serikali kusaidia ikiwemo nishati ya umeme na masuala ya kikodi kuchukua muda mrefu kupatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema Serikali imedhamiria kuendelea kuweka mazingira rafiki ili kuwezesha shughuli za madini kufanyika na kuleta matokeo  kutokana na umuhimu wa Sekta ya Madini katika maendeleo ya  kiuchumi.

Aidha, Dkt. Kiruswa amemweleza Mkurugenzi huyo kuhusu hatua mbalimbali ambazo Serikali inaendelea kuzichukua kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere ambalo kukamilika kwake litazalisha Megawati 2,115.

Pia, Dkt. Kiruswa ametoa ushauri kwa  kampuni za madini kuwa na utaratibu wa kukutana na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa taarifa za utekelezaji Wa miradi ili kuweka uelewa wa pamoja Kwa wananchi na kuongeza kuwa Wizara Iko tayari kushirikia na kampuni hizo.

Mgodi wa Mwadui ni wa ubia kati ya Kampuni ya Williamson Diamonds yenye umiliki wa hisa zipatazo 63 na  Serikali inamiliki asilimia 37 kutoka  asilimia 25 za awali.

Katika hatua nyingine, Viongozi na Watendaji wa Wizara wameendekea kukutana na kampuni mbalimbali.

#TANZANIA
@TheMiningIndaba

#InvestInTanzaniaMiningSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals