[Latest Updates]: Buckreef Yakonga Moyo wa Waziri Biteko kwa Kutoa Ajira kwa Wazawa

Tarehe : July 16, 2022, 8:59 a.m.
left

WAZIRI wa Madini, Dkt. Doto Biteko ameupongeza mgodi wa dhahabu wa Buckreef kwa kutoa ajira kwa Watanzania wanaofanya kazi mbalimbali za uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo.

Dkt. Biteko amebainisha hayo Julai 16, 2022 wakati alipotembelea mgodi wa Buckreef mkoani Geita ili kujionea maendeleo ya shughuli za ujenzi na uchimbaji madini katika mgodi huo. 

Amesema, mgodi wa Buckreef umetoa ajira za moja kwa moja 354 kwa Watanzania katika nafasi mbalimbali katika mgodi huo.

Amesisitiza kwa wafanyakazi waliopewa ajira katika mgodi huo kuhakikisha wanajenga taswira nzuri kwa kuwa wazalendo na waaminifu katika kazi zao. 

Amesema, kupitia uaminifu wawekezaji watatoa fursa zaidi kwa Watanzania kuweza kufanya kazi mbalimbali.

Aidha, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, miradi yote iliyopo kwenye Sekta ya Madini itaendelezwa ili watanzania wanufaike na rasilimali madini na kuongeza Pato la Taifa. 

"Matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kwamba miradi yote ambayo ipo kwenye Sekta ya Madini iweze kuendelezwa,"amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkuu Mkoa wa Geita Rosemary ameupongeza mgodi wa Buckreef kwa kusimamia usalama kwa wafanyakazi. 

Aidha, amemuomba Dkt. Biteko kuhakakisha Serikali inaleta wawekezaji wengi mkoani Geita kutokana na mkoa huo kuwa na maeneo mengi ya uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Naye, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buckreef Gaston Mujwahuzi amesema wataendelea kuwashirikisha wananchi katika huduma za kijamii kwa ajili ya manufaa ya watu wote. 

Aidha, shughuli nyingi za manunuzi ya vifaa mbalimbali yanafanyika hapa nchini ili kuhakikisha manufaa ya uwekezaji yanabaki kuwa ya watanzania.

Kampuni ya Dhahabu ya Buckreef ikishirikiana na mbia mwenza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inajushughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu. Pia Kampuni ya Buckreef inamiliki hisa kwa asilimia 55 na STAMICO inamiliki hisa asilimia 45.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals