[Latest News]: Sekta ya Madini Yaendelea Kufanya Mapinduzi Makubwa ya Kiuchumi Nchini

Tarehe : Nov. 3, 2025, 3:27 p.m.
left

Dodoma

Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa (GDP) umeongezeka na kufikia  kiwango cha asilimiam10.1 mwaka 2024 ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya mwaka wa 2025. Hii ni kutokana na  juhudi mbalimbali za kisekta zinazoendelea kufanya mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi  ikiwa pamoja na kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za  kiuchumi nchini. 

Juhudi hizo za mafanikio zinaendelea kuleta mafanikio ambapo katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2024/2025, sekta ya madini iliwekewa lengo la kukusanya shilingi trilioni 1 , lakini hadi kufikia Mei 24 ,2025, tayari ilifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 930 ikiwa ni mafanikio makubwa kabla ya mwaka wa fedha kumalizika.

Kufuatia marekebisho ya Sheria ya Madini mwaka 2024, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilianza rasmi kununua dhahabu kutoka kwa wazalishaji wa ndani. Sheria sasa inawataka wamiliki wote wa leseni za uchimbaji wa dhahabu kutenga angalau asilimia 20 ya uzalishaji wao kwa ajili ya kuuza BoT. Kuanzia Oktoba 2024 hadi sasa (miezi 8), BoT iliweza kununua tani 3.7 za dhahabu. 

Kwa hatua hii, Tanzania inajiweka kwenye nafasi nzuri kuwa miongoni mwa nchi zenye akiba kubwa ya dhahabu barani Afrika mfano, hivisasa Algeria barani Afrika inaongoza kwa kuwa na akiba ya tani 174, na Msumbiji iko nafasi ya 10 kwa tani 3.6. 

Katika kuendeleza ushiriki wa masoko ya ndani ya wazi, Serikali ilirejesha rasmi minada ya ndani ya madini ya vito kwa lengo la kuongeza thamani ya madini haya, hasa Tanzanite ambayo ni adimu duniani , katika kipindi husika Serikali ilifanikiwa kuendesha minada Mirerani mwezi Desemba 2024 na Arusha Februari 2025, juhudi hizi pia ni sehemu ya kujenga sura mpya ya Tanzanite ili kutambulika zaidi kimataifa.

Kuhusu ajira kwa Watanzania kupitia  sekta ya madini zimeongezeka. Kwa sasa ajira za moja kwa moja ni zaidi ya 19,356, ambapo asilimia 97 ya ajira hizo ni kwa Watanzania. Sambamba na hapo, Watanzania pia wanaendelea kushikilia nafasi nyingi za juu kwenye migodi pamoja na kutoa huduma muhimu kama vile utengenezaji wa vifaa vya migodini, hatua ambayo inachochea uchumi wa ndani.

Serikali imeimarisha upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa wachimbaji wadogo kupitia vituo vya ununuzi wa madini. Hatua hii inalenga kuwapa wachimbaji bei nzuri, kuwasaidia kupata mapato ya haki na kudhibiti utoroshaji wa madini nje ya mfumo rasmi, mpaka sasa kuna masoko 44 nchi nzima na Vituo vya Ununuzi 114.

Kwa upande wa mahusiano ya Kimataifa Wizara ya Madini kwa kushirikiana Taasisi zake imefanikiwa kusaini mikataba ya ushirikiano na nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza (UK), Sweden, Finland na nyingine nyingi kwa ajili ya kukuza ujuzi, teknolojia na kupata mitaji kwa ajili ya maendeleo ya sekta kwa manufaa ya taifa .

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals