[Latest Updates]: Wananchi Msijifungie Ndani, Jifunzeni Kupitia Maonesho ya Geita – Mtaalamu wa Wizara

Tarehe : Sept. 25, 2025, 11:05 a.m.
left

Asema Ni Jukwaa la Kujifunza na Kushiriki Mnyororo wa Uchumi wa Madini”

 Geita

Kufuatia uwepo wa fursa lukuki zilizopo katika Sekta ya Madini nchini, wananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa jirani wameaswa kutembelea Maonesho ya 8 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea ili kujifunza na hatimaye kushiriki katika uchumi wa madini kupitia nyanja mbalimbali.

Wito huo umetolewa na Mjiolojia kutoka Wizara ya Madini, Benjamin Mikomangwa, katika mahojiano maalum na Radio Inlandya Mwanza ambapo amewasihi wananchi na wadau kutobaki majumbani kwa kuwa maonesho hayo yanaelimisha kuhusu shughuli mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo mzima wa madini, ikiwemo huduma zinazotolewa na taasisi za wizara na wadau.

“Kwa mfano, taasisi zote za Wizara zinashiriki maonesho haya. Chukulia mfano wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kinachotoa mafunzo ya uongezaji thamani wa madini ya vito. Hii ni fursa muhimu ya watu kujifunza kutokana na umuhimu wa kuongeza thamani ya madini, jambo ambalo ni takwa la Sera ya Madini ya mwaka 2009. Kwa sasa Serikali imeweka msukumo mkubwa kuhakikisha madini yanaongezwa thamani hapa nchini kabla ya kusafirishwa nje,” amesisitiza Mikomangwa.

Ameongeza kuwa, lengo la Serikali ni kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi ili kuongeza fursa za ajira, mapato ya sekta na mchango wake katika pato la taifa.

Aidha, Mikomangwa amesema wananchi wanapaswa kuutumia Mkoa wa Geita kama mfano wa kujifunza kupitia maonesho hayo, kutokana na namna ulivyojipambanua kupitia shughuli za uchimbaji, hususan wa dhahabu, ambapo Geita inaongoza kitaifa kwa uzalishaji wa madini hayo. Amesisitiza kuwa wananchi hawapaswi kujifungia ndani, bali kuyatumia maonesho hayo kama jukwaa muhimu la kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Mikomangwa amesema Wizara inaendelea kutekeleza vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2025/26, huku msukumo ukiwekwa kuhakikisha malengo yaliyopangwa na Serikali, yakiwemo ukusanyaji wa maduhuli, yanafikiwa.

“Katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ilivuka lengo la makusanyo kwa kukusanya shilingi trilioni 1.183. Mwaka huu Serikali imetupangia kukusanya shilingi trilioni 1.405. Nina imani tutafikia malengo hayo kama tulivyofanikiwa kuchangia asilimia 10.1 ya Pato la Taifa mwaka 2024, kabla ya lengo la mwaka 2025,” amesema Mikomangwa.

Mara kadhaa, Wizara imekuwa ikihamasisha wananchi kushiriki katika uchumi wa madini kupitia fursa mbalimbali zilizopo. Hili pia liliwekwa msisitizo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, alipofungua maonesho hayo Septemba 22, 2025, ambapo alisema Sekta ya Madini ni mhimili unaobeba uchumi wa Kanda ya Ziwa na taifa kwa ujumla, na akaitaka jamii kushiriki kikamilifu katika fursa zinazojitokeza kupitia sekta hiyo.

#Vision2030: Madini ni Maisha na Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals